Connect with us

General News

Chebukati awataka Wakenya kujitokeza kwa shughuli ya usajili wa wapigakura wapya, awamu ya pili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chebukati awataka Wakenya kujitokeza kwa shughuli ya usajili wa wapigakura wapya, awamu ya pili – Taifa Leo

Chebukati awataka Wakenya kujitokeza kwa shughuli ya usajili wa wapigakura wapya, awamu ya pili

Na CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuwa wapigakura katika awamu ya pili inayoanza mwezi huu Januari.

Kwenye taarifa yake ya mwaka mpya wa 2022, Bw Chebukati pia aliwahimiza wanasiasa kuendesha kampeni kwa amani.

“Awamu ya pili ya usajili wa wapigakura wapya na usajili huo katika mataifa ya ng’ambo inaanza mwezi huu. Kwa hivyo, natoa wito wa wale ambao hawajasajiliwa kujitokeza kwa wingi ili wajisajili,” Bw Chebukati akasema.

Katika awamu ya kwanza ya shughuli hiyo iliyofanyika kuanzia Oktoba 5, 2021 hadi Novemba 15, 2021, IEBC iliweza kuwasajili Wakenya 1.5 milioni pekee ilhali ililenga kuwasajili watu milioni sita.

Japo tume hiyo ililaumiwa kwa kutoendesha uhamasisho tosha kuhusu shughuli hiyo, ilibainika kuwa Wakenya wengi, haswa vijana hawakuwa na msukumo wa kushiriki shughuli hiyo.

Lakini IEBC ilijitetea kwamba haikuwa na fedha za kuiwezesha kuendesha uhamasisho huo kwa sababu Hazina ya Kitaifa haikutoa fedha za kutosha.

Vile vile, Bw Chebukati na makamishna wenzake walisema hali hiyo ilitokana na hatua ya serikali kuu kuzima mashirika ya kigeni kufadhili shughuli za uchaguzi kupitia tume hiyo au mashirika ya kijamii.

Kuhusu kampeni za amani, Bw Chebukati alisema huo ni wajibu wa wanasiasa na Wakenya wote kwa ujumla.

“Ni katika mazingira ya amani ambapo tutaweza kuendesha uchaguzi kwa njia huru na haki na ambayo matokeo yake yataaminika,” akaeleza huku akitoa hakikisha kuwa IEBC inajitolea kufanikisha hilo.

Bw Chebukati aliongeza kuwa tume hiyo itaendelea kushauriana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa imefanikiwa na kuendesha uchaguzi huo wa Agosti 9, 2022 kwa njia huru.

“Ni kupitia ushirikiano na wadau hao ambapo matokeo ya uchaguzi huo yataaminika na washiriki wote,” akaeleza.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending