[ad_1]
Chelsea walaza Newcastle United ligini
Na MASHIRIKA
CHELSEA walikomoa Newcastle United 1-0 katika mchuano wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugani Stamford Bridge tangu mmiliki wao Roman Abramovich awekewe vikwazo na serikali ya Uingereza.
Mechi hiyo ilionekana kukamilika kwa sare tasa kabla ya kiungo mvamizi Kai Harvetz kufungia Chelsea bao la pekee na la ushindi katika dakika ya 88.
Bao hilo lilikuwa la uchungu zaidi kwa Newcastle ikizingatiwa kwamba walitaka refa amfurushe Harvetz uwanjani katika kipindi cha kwanza kwa hatia ya kumpiga kumbo beki Dan Burn.
Kabla ya bao, timu zote zilikuwa na wakati mgumu kupata nafasi za kufunga magoli huku Chelsea wakilazimika kusubiri hadi dakika ya 75 ili kuelekeza kombora lililolenga shabaha kwenye goli la wageni wao.
Chini ya kocha Thomas Tuchel, Chelsea kwa sasa wanakamata nafasi ya tatu kwenye jedwali la EPL kwa alama 59 kutokana na mechi 28 ambazo pia zimetandazwa na nambari mbili Liverpool (alama 66) na mabingwa watetezi Manchester City wanaoselelea kileleni kwa pointi 69. Newcastle wanashikilia nafasi ya 14 kwa alama 31.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
WANTO WARUI: Taratibu zote zifuatwe katika usahisishaji…
[ad_2]
Source link