Connect with us

General News

Chelsea warefusha mkataba wa beki Thiago Silva kwa mwaka mmoja – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chelsea warefusha mkataba wa beki Thiago Silva kwa mwaka mmoja – Taifa Leo

Chelsea warefusha mkataba wa beki Thiago Silva kwa mwaka mmoja

Na MASHIRIKA

CHELSEA wamerefusha mkataba wa mwanasoka Thiago Silva kwa mwaka mmoja zaidi hadi mwisho wa msimu wa 2022-23.

Beki huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 37 amechezea Chelsea mara 22 hadi kufikia sasa muhula huu wa 2021-22.

Silva alikuwa sehemu ya mabeki wakuu waliotegemewa na Chelsea kwenye fainali iliyowashuhudia wakitandika Manchester City na hatimaye kutwaa ufalme wa Klabu Bingwa Ulaya mnamo Mei 2021.

Tangu atue uwanjani Stamford Bridge baada ya kusajiliwa kutoka Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa bila ada yoyote mnamo Agosti 2020, Silva amefungia Chelsea mabao manne.

“Nilidhani sitawahi kuchezea Chelsea kwa miaka mitatu. Nina furaha na ninahisi kustahiwa pakubwa kutokana na fursa hii ya kusakatia miamba hawa kwa msimu mmoja zaidi,” akasema Silva aliyetandaza mchuano wake wa 100 katika timu ya taifa ya Brazil mnamo Oktoba 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending