Connect with us

General News

Conte ashinda mechi yake ya kwanza akidhibiti mikoba ya Spurs – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Conte ashinda mechi yake ya kwanza akidhibiti mikoba ya Spurs

Conte ashinda mechi yake ya kwanza akidhibiti mikoba ya Spurs

Na MASHIRIKA

KOCHA Antonio Conte alisajili ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) akidhibiti mikoba ya Tottenham Hotspur baada ya masogora wake kutoka nyuma na kupepeta Leeds United 2-1 mnamo Jumapili usiku.

Spurs walianza mchezo kwa matao ya chini huku wakishindwa kuvurumisha kombora lolote langoni mwa Leeds United walioshambulia sana kupitia Kalvin Phillips na Adam Forshaw waliomtatiza kipa Hugo Lloris.

Daniel James aliwaweka Leeds kifua mbele mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kujaza kimiani krosi ya Jack Harrison. Baada ya kuzomewa na mashabiki walipokuwa wakiondoka uwanjani baada ya dakika 45 za kwanza, wanasoka wa Spurs walirejea ugani wakiwa na ari ya kushinda mechi katika kipindi cha pili. Harry Kane na Song Heung-min walishuhudia fataki zao zikigonga mwamba wa goli la Leeds.

Pierre-Emile Hojbjerg aliwafungulia Spurs ukurasa wa mabao katika dakika ya 58 baada ya kushirikiana na Lucas Moura. Bao la pili la kikosi hicho cha Conte lilifungwa na Sergio Reguilon aliyekamilisha krosi ya Eric Dier.

Goli hilo lilikuwa la kwanza kwa Reguilon kufungia Spurs waliopaa hadi nafasi ya saba kwa alama 19 sawa na Wolves. Ni pengo la alama nne pekee ndilo linatenganisha Spurs na West Ham United wanaofunga mduara wa nne-bora jedwalini.

Leeds wanakamata nafasi ya 17 kwa alama 11, tano zaidi kuliko Newcastle United wanaovuta mkia.