[ad_1]
Corona iligeuza Wakenya ombaomba – Ripoti
Na BRIAN AMBANI
Wakenya wengi waliomba msaada wa kifedha kutoka kwa jamaa zao walio ng’ambo baada ya kupoteza ajira kufuatia janga la virusi vya corona miaka miwili iliyopita.
Ripoti ya Benki Kuu Nchini (CBK) inaonyesha kuwa hata mapato ya Wakenya hao wanaoishi ughaibuni pia yaliathiriwa huku kiwango cha wastani cha fedha kila mmoja wao mwaka huo alituma nchini kikipungua kutoka Sh681,000 mnamo 2019 kabla ya ujio wa corona hadi Sh454,000 mnamo 2020.
Kando na kusababisha Wakenya wengi kupoteza ajira, baadhi mishahara yao ilipunguzwa na waajiri wao huku idadi ya walioomba msaada kwa jamaa zao nje ya nchi ikipanda maradufu.
Shirika la Taifa la Takwimu Nchini (KNBS) lina data iliyoonyesha kuwa Wakenya 1.72 milioni walipoteza ajira kwa muda wa miezi mitatu hadi Juni 2020 wakati ambapo serikali ilifunga nchi kama mojawapo ya mikakati ya kuzuia kuenea kwa janga la corona.
Mwaka huo, idadi ya Wakenya waliokuwa wameajiriwa ilipungua kutok 17.59 milioni hadi 15.87 milioni huku kampuni nyingi zikilemewa kulipa mishahara kikamilifu.
Hata hivyo,hali kwa sasa hali ya kawaida inaendelea kurejea nchini baada ya serikali kuondoa kafyu mwaka jana na pia baadhi ya kampuni kuwarejesha kazini wafanyakazi wao huku wengine wakirejeshewa mishahara kikamilifu.
Kulingana na ripoti ya CBK Wakenya ambao wapo ng’ambo walituma fedha kupitia benki mbalimbali, simu na njia nyingine za kuhamisha fedha ili kuwafaa wenzao japo hata chumi za nchi ambako walikuwa pia ziliathirika.
Pesa hizo ambazo zilikuwa zikitumwa kila mwezi zilikuwa za kuwasaidia jamaa zao kujikimu kimaisha kwa kununua vyakula, dawa, kulipia watoto wao karo pamoja na mahitaji mengine ya kimsingi.
Ripoti ya CBK inakuja wakati ambapo ilibainika kuwa mwaka jana pekee, Wakenya wanaoishi ng’ambo walituma Sh39.75 bilioni mwezi uliopita pekee huku uchumi wa nchi nyingi barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Marekani ukiendelea kuinuka.
Next article
TUSIJE TUKASAHAU: Serikali yafaa kufuata sheria za…
[ad_2]
Source link