Wizara ya Afya imetangaza maambukizi 403 mapya ya COVID-19, na kiwango cha chanya kimefika asilimia 7.2 % baada ya sampuli 5,577 kupimwa katika saa 24 zilizopita.
Kulingana na Wizara ya afya idadi ya wagonjwa nchini Kenya imefika 175,176 kutokana na sampuli 1,864,020 zilizopimwa tangu mwezi Machi 2020 kisa cha kwanza kilipotua nchini.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akihutubu hapo awali. Picha: MoH. Source: Facebook
Watu 399 walioambukizwa ni Wakenya nao 4 ni raia wa kigeni; 215 ni wagonjwa wa kiume nao 188 ni wa kike.
Mgonjwa mchanga zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja, naye mkongwe ana miaka 97.
Jumla ya wagonjwa 957 kwa sasa wamelazwa katika vituo anuwai vya afya nchini kote, wakati wagonjwa 4,796 nao wametengwa nyumbani wakipokea huduma za matibabu.
Wakati huo huo, Wizara ya Afya iliripoti kuwa wagonjwa 442 wamepona, na 24 walitoka katika vituo mbali mbali vya afya nchini na 418 wengine walikuwa wakihudumiwa nyumbani.
Idadi ya walipata nafuu sasa iimegonga 120,031, na 87,288 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani mwao nao 32,473 kutoka vituo vya afya.
Aidha watu wengine 18 waliripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na makali ya maradhi hayo, ambapo sasa idadi ya waliofariki dunia 3,378.