Connect with us

General News

Dada wawili kushtakiwa kushambulia pacha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Dada wawili kushtakiwa kushambulia pacha – Taifa Leo

Dada wawili kushtakiwa kushambulia pacha

Na RICHARD MUNGUTI

DADA wawili waliodai walichapwa na kujeruhiwa na ndugu pacha katika hoteli moja jijini Nairobi Oktoba 2021, walisema Jumatatu wako tayari kujibu mashtaka.

Kupitia kwa wakili Philip Murgor anayewakilisha dada hao Stephanie Murgor na Cheryl Murgor, walisema wako tayari kufika kortini lakini akaeleza masikitiko yake jinsi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji amekosa kusimamia haki katika kesi hiyo.

Katika mahojiano na Taifa Leo Bw Murgor alisema agizo la Bw Haji kwamba dada hao washtakiwe ni thibitisho kwamba hawezi watetea wahasiriwa wa dhuluma za jinsia.

“Agizo la Bw Haji kwamba Stephanie na Cherly washtakiwe ilhali ni wao waliojeruhiwa ni sababu tosha DPP huyu hawezi akawatetea wahasiriwa wa dhuluma za kijinsia (GBV),” Bw Murgor alisema.

Na wakati huo huo, chama cha mawakili wanawake nchini (Fida) kimeandikia afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kikilalamika jinsi uchunguzi wa kesi hiyo ulivyofanywa.

Chama hicho kimeomba agizo dada hao washtakiwe lisitishwe kisha uchunguzi katika kisa hiyo uchunguzwe upya.

Barua hiyo ilipokelewa na naibu msaidizi wa DPP Joseph Riungu.

Fida kimesema ni jambo la kusikitisha kwamba wahasiriwa wamegeuzwa kuwa washtakiwa.

Bw Murgor alisema dada hao walilazimishwa na ODPP kuondoa madai dhidi ya Paul Mwaura Ndichu na nduguye Edward Wanyoike Ndichu lakini wakakataa.

Mwaura na Wanyoike walidaiwa walichapa na kuwaumiza dada hao usiku wa Oktoba 16/17 2021 katika hoteli moja jijini Nairobi saa tisa usiku wa manane.

Murgor amehoji kuvurugwa kwa video za CCTV ambapo ndugu hao walikuwa wanatisha kuwapiga risasi dada hao.