DP William Ruto alisema mageuzi ambayo yamekuwa yakifanywa na Uhuru ndani ya Jubilee ni kuwalenga marafiki wake. Picha: William Ruto Source: Facebook
Akiongea nyumbani kwake Sugoi kaunti hya Uasin Gishu, Ruto alisema kumekuwa na vitisho vingi kwa wote ambao wanamuunga mkono.
Aliwataka viongozi wa kanisa kumuombea pamoja na wandani wake ili waweze kushinda vita dhidi ya mahasimu wao.
“Wanatishwa watapelekwa mahakamani, EACC, KRA, kutolewa kutoka afisi hii na ile na si kwa sababu wameshindwa kufanya kazi lakini kwa sababu ni marafiki wa naibu rais wa Kenya,” alisema DP.
“Muombee huyu shetani anakuja kuleta mgawanyiko ili Mungu atausaidie kuleta umoja. Na mutuombee sisi viongozi tusirudishe Kenya kwenye siasa za mgawanyiko na ukabila,” alisema Ruto.
Ilikuwa mara ya kwanza DP kuzungumzia waziwazi masaibu ambayo yamekuwa yakiwapata wandani wake.
Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akifanya mabadiliko ndani ya chama cha Jubilee ambao wote ni marafiki wa DP wametolewa kwenye nyadhifa walizoshikilia.
Aliyekuwa kiongozi wa wengi Aden Duale. Aliondolewa kutoka wadhifa wake kwa madai kuwa ni mwandani wa DP. Picha: Nation Source: Facebook
Aliyekuwa kiongozi wa wengi Aden Duale aliondolewa kutoka wadhifa wake kwa madai kuwa ni mwandani wa DP.
Wengine ambao wameangukiwa na shoka la Rais Uhuru ni aliyekuwa kiongozi wa wengi kwenye Seneti Kipchumba Murkomen.
“Naibu rais amezungumza kwa niaba yetu wote. Tutakuwa wavumilivu na tutamshinda pepo wa chuki na mgawanyiko,” Murkomen alisema baada ya DP kuteta wandani wake kuhangaishwa.