Connect with us

General News

DRC yachemkia Ruto – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

DRC yachemkia Ruto – Taifa Leo

DRC yachemkia Ruto

NA CHARLES WASONGA

NAIBU Rais William Ruto ameshambuliwa vikali na viongozi na raia wa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo (DRC) kutokana na madai yake kwamba nchi hiyo haina ng’ombe wa maziwa.

Dkt Ruto alitoa kauli hio Jumatatu wiki katika Kaunti ya Nyeri alipoongoza mkutano wa majadiliano kuhusu mfumo wa kiuchumi anaopendekeza wa “Bottom Up”.

“Kuna soko kubwa zaidi la maziwa nchini DRC kwa sababu taifa hilo lenye jumla ya watu 90 milioni halina hata ng’ombe mmoja wa maziwa,” akasema katika ushauri wake kwa wakazi kuzidisha uzalisha za maziwa.

“Ndio, narudia kuwa kuna soko kubwa huko kwa wale watu hucheza muziki wakivalia long’i kwa tumbo,” Dkt Ruto akaongeza.

Kauli hiyo iliwakasirisha wanasiasa, wanahabari, watetezi wa haki na raia wa DRC ambao walimshutumu Naibu Rais kwa kuonyesha dharau kubwa kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Seneta wa DRC Balozi Francine Muyumba Nkanga alimtaka Dkt Ruto kuondoa matamshi hayo, na kuomba masamaha, akidai yanaweza kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na taifa hilo ambalo linatarajiwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Naibu Rais William Ruto, hii haifai na hatukubali. Ondoa dai hili kwamba DRC haina ng’ombe wa maziwa. Ikiwa DRC haina hata ng’ombe mmoja wa maziwa mbona Kenya ilitia saini mikataba ya kibiashara na Benki ya Equity wakati huu inatengeza pesa nchini mwetu. Hii ni matusi,” Bi Mayumba akasema kupitia Twitter.

Seneta huyo vile vile, alitisha kuchukua hatua dhidi ya Kenya kwa kuwasilisha suala hilo katika Bunge la DRC.

Mwenyekiti wa muungano wa vyama vya wachimbaji madini DRC Jean Paul Ilunga alitaja kauli ya Dkt Ruto kama tusi kwa nchi yake.

“Hatuko tayari kukubali tusi hili. Naibu Rais William Ruto lazima aheshimu nchi za eneo hili hasa DRC. Ninahakika atapoteza kura nyingi. Muziki ni shughuli katika kila nchi,” alisema Bw Ilunga.

Joto kuhusu matamshi ya Ruto yalifanya raia wa DRC kususia huduma katika benki ya Equity jijini Kinshasa jana.

Hii ilifanya balozi wa Kenya nchini DRC George Masafu kusema kuwa suala hili limeibua kero kubwa miongoni mwa wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

“Ubalozi wa Kenya hapa umejulisha Wizara ya Mashauri ya Kigeni Nairobi Kenya kuhusu joto lililosababishwa na matashi ya Bw William Ruto,” akasema Dkt Masafu kwenye taarifa kwa vyombo vya habari na kuongeza hayawakilishi msimamo wa Kenya.

Mnamo Aprili 21, 2022 Rais wa DRC Felix Tshisekedi alizuru Kenya ambapo pamoja na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta walitia saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.