Kila siku ya wiki, TUKO.co.ke inakupakulia kwa mukhtasari matukio na habari muhimu zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ili ukapate kufahamu kwa upana na utendeti mambo yalivyo ulimwenguni.
Gavana Anne Mumbi Waiguru Jumatano, Juni 24, aliambia kamati teule ya seneti kuwa alitimuliwa kwa sababu ya kuunga mkono ripoti ya BBI.
Waiguru alisema hakuna ushahidi ambao uliwasilishwa mbeleya kamati hiyo na kwa hivyo ni siasa za kitaifa.

Waiguru alipofika mbele ya kamati ya Seneti. Picha: UGC.
Source: Facebook
Runinga ya K24 ambayo inamilikiwa na shirika la utangazaji la Media Max imewafuta kazi ghafla wafanyakazi zaidi ya 100.
Mtangazaji Nancy Onyancha pamoja na mumewe Joab Mwaura ambao walikuwa wakifanya kazi katika shirika hilo ni miongoni mwa wale waliopigwa kalamu.

Nancy Onyancha na mumewe Joab Mwaura.Picha: Nancy Onyancha.
Source: UGC
Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru aliwashangaza Wakenya mitandaoni baada ya picha kadhaa kuenezwa zikimuonyesha akishiriki mchezo wa kadi almaarufu ‘Solitaire’ kwenye simu yake.
Waiguru alikuwa akicheza mchezo huo wakati kesi dhidi yake ya kumfurusha mamlakani ilipokuwa ikisikizwa katika bunge la seneti.

Waiguru anaswa kwenye picha akichezo mchezo wa solitaire.Picha: The Star.
Source: UGC
4. Jalang’o aondoka Milele FM
Mcheshi Felix Odiwuor maarufu kama Jalang’o amejiuzulu kutoka kazi yake ya kifahari ya Milele FM.
Jalang’o alitangaza haya kupitia kurasa zake mtandaoni Jumatatu, Juni 22.
Mwanasiasa mkongwe, Nazlin Umar ameonekana kufurahia kung’olewa kwa Aden Duale kama Kiongozi wa Wengi Bunge la Kitaifa.
Umar, ambaye awali penyenye zilidai kwamba alikuwa katika uhusiano wa mapenzi na Duale, alishindwa kuficha bashasha yake kufuatia masaibu ya Duale.

Picha ya Dan Duale na Nazlin Umar. Picha: UGC.
Source: UGC
Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale alondolewa katika wadhifa wa Kiongozi wa Wengi Bungeni na nafasi hiyo kukabidhiwa Mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya.

Aden Duale alitwaliwa na Mbunge Amos Kimunya.
Source: UGC
Aliyekuwa waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri amesajili chama chake cha kisiasa tayari kwa mirindimo ya 2022.
Kulingana na kaimu msajili wa vyama Ann Nderitu, Kiunjuri amesajili chama cha The Service Party.

Mwangi Kiunjuri amekuwa akionekana kuwa mwandani wa Naibu Rais William Ruto kwenye siasa za 2022. Picha: William Ruto.
Source: UGC
Mwanamziki Betty Bayo Jumapili, Juni 21 aliwasisimua wanamtandao baada ya kumtumia aliyekuwa mumewe mhubiri Victor Kanyari ujumbe wenye utani siku ya kusherekea kina baba.

Betty Bayo alimtumia aliyekuwa mumewe ujumbe wenye utani siku ya kusherekea kina baba.
Source: UGC