Connect with us

General News

EACC yaagiza madiwani kurudisha pesa ‘walizopora’ Mombasa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

EACC yaagiza madiwani kurudisha pesa ‘walizopora’ Mombasa – Taifa Leo

EACC yaagiza madiwani kurudisha pesa ‘walizopora’ Mombasa

NA GEORGE ODIWUOR

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewaa – giza madiwani katika Bunge la Kaunti ya Homa Bay kurudisha fedha walizolipwa kama marupurupu kinyume cha sheria kwenye ziara moja waliyofanya jijini Mombasa mwaka uliopita.

Kando na madiwani, maafisa wa ngazi za juu katika kaunti pia walipewa marupurupu hayo. Tume ilianza uchunguzi kuanzia Desemba mwaka uliopita, baada ya kubaini madiwani 25 na wafanyakazi wa bunge hilo walipokea marupurupu ambayo hayakulingana na majukumu yaliyowapeleka huko.

Tukio hilo ni moja ya kesi ambazo zimekuwa zikichunguzwa na tume hiyo.

Kesi nyingine inayochunguzwa ni mkataba kati ya Bodi ya Uajiri ya Bunge la Kaunti na kampuni ya M/S Hartland Enterprises Limited, kuhusu ujenzi wa afisi ya bunge hilo.

Tume ilimaliza uchunguzi kuhusu kesi ya kwanza na kuwaagiza madiwani waliolipwa pesa zilizozidi kiwango walichopaswa kulipwa kuzirudisha. Waliagizwa kuziweka kwenye Akaunti ya Tume ya Kunasa Mali Iliyoporwa.

Madiwani waliohojiwa kuhusu kesi hizo mbili ni Ellyphalet Osuri (Ruma Kaksingri) Walter Were (Kanyadoto), David Oloo (Kologi), Geoffrey Opiyo (Kasipul Kusini), Okuku Miregi (Rusinga), Philmon Okombo (Gembe), Joan Ogada (Kojwach), Michael Odira ( Kibiri), Bob Obondo ( Kasipul ya Kati), Paul Wamunga (Karachuonyo Kaskazini) na Ellyas Orondo (Gem Mashariki).

Wengine ni madiwani maalum Amina Osmail, Pamela Odira, Lorna Owino, Judith Kamaria, Monoflorita Ondiek, Kevin Onyango, Jane Kiche, Mary Gaya, Nelly Odek, Ruth Ombura na Sophy Salim.

Madiwani hao walidaiwa kusafiri Mombasa kati ya Septemba 8 na 12 2021, ambapo walilipwa marupurupu ya siku tano ilhali ziara hiyo ilidumu kwa siku mbili pekee.