Aliyekuwa gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua. Bunge la kaunti ya Nakuru limependekeza achunguzwe na EACC. Picha: Standard Source: Facebook
Ripoti hiyo ilipendekeza Mbugua achunguzwe na tume ya kukabiliana na ufisadi EACC kuhusu fedha hizo kwenye bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2015/16.
“Kamati hii inapendekeza EACC ifanye uchunguzi uwezekano wa ukora, wizi na matumizi mabaya ya fedha hizo kima cha KSh 3.5bn,” EACC ilisema.
Ripoti hiyo ya PAIC ilitokana na ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambaye alisema kaunti hiyo ililipa KSh 1.5bn lakini hakukuwa na stakabadhi za kuonyesha ulipaji huo.