Connect with us

General News

Ecowas yawashinikiza wanajeshi nchini Mali – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ecowas yawashinikiza wanajeshi nchini Mali – Taifa Leo

Ecowas yawashinikiza wanajeshi nchini Mali

Na KEMO CHAM

BAMAKO, MALI

JUMUIYA ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza vikwazo vikali dhidi ya Mali, baada ya utawala wake wa kijeshi kukosa kubuni serikali ya mpito ya kiraia katika muda iliyopewa.

Kwenye taarifa Jumatatu, jumuiya hiyo iliziagiza nchi 16 wanachama wake kutoshirikiana na Mali kwa shughuli yoyote ile.

ECOWAS Iliyaagiza mataifa hayo kufunga mipaka yake ya ardhini na angani, na kusimamisha ushirikiano wowote wa kibiashara.

Uamuzi huo ulifikiwa na viongozi wa mataifa hayo kwenye kikao cha dharura kilichofanyika Jumapili jijini Accra, Ghana.

Viongozi hao pia waliagiza taasisi zote za kifedha katika nchi zao kufunga akaunti zote za Mali na kusimamisha usaidizi wowote wa kifedha kwa taifa hilo.

Hata hivyo, agizo hilo lilitoa mwanya kwa mataifa hayo kusafirisha bidhaa muhimu kama vyakula, dawa na chanjo za kukabiliana na virusi vya corona.

Kikao hicho kilifanyika siku chache baada ya utawala huo kutangaza mpango mpya wa kiutawala ambao unakiuka ule uliokuwa umetangazwa na ECOWAS.

Jumuiya hiyo ilikuwa imeupa utawala huo makataa ya hadi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kubuni utawala wa mpito unaoongozwa na raia.

Mali imekuwa kwenye mzozo na Ecowas kutokana na mapinduzi mawili ya kijeshi ambayo yametokea katika taifa hilo katika muda wa miaka miwili iliyopita.

Mzozo huo ulianza Agosti 2020, baada ya kundi la wanajeshi lililoongozwa na Kanali Assimi Goita kuipindua serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Ibrahim Boubacar Keita.

Miezi tisa baadaye, wanajeshi hao walifanya mapinduzi ya pili kwa kuuondoa utawala wa kiraia waliokuwa wamebuni baada ya kupokea vitisho vya kuwekewa vikwazo.

Baada ya mapinduzi hayo, utawala huo ulipewa makataa ya miezi 18 kuandaa uchaguzi na kukabidhi mamlaka kwa utawala wa kiraia.

Hata hivyo, utawala huo unashikilia kuwa muda huo hautoshi kwake kutimiza masharti hayo.

Wiki iliyopita, utawala huo ulibuni mpango wake ambao unapendekeza muda wa hadi miaka mitano kukabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.

Viongozi wa jumuiya hiyo walitaja mpango huo kuwa “usiokubalika”, kwani “unamaanisha utawala huo utaendelea kuwashika mateka raia wa taifa hilo.”

Jumuiya hiyo ilitoa vikwazo kwa mara ya kwanza kwa utawala huo Novemba 7, 2021, baada yake kuanza kuonyesha dalili za kukiuka masharti uliyokuwa umepewa.

Karibu viongozi 150 wa utawala huo waliwekewa vikwazo, baadhi vikiwa akaunti zao kufungwa na marufuku ya kusafiri.

Kulingana na agizo la Jumapili, vikwazo hivyo vipya vitatekelezwa pamoja na vile vya kiuchumi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending