[ad_1]
EPL na FA zakatiza dili ya mechi zao kupeperushwa nchini Urusi
Na MASHIRIKA
VINARA wa Ligi Kuu ya Uingereza wameahirisha dili kati yao na Urusi ya kupeperusha matangazo ya moja kwa moja ya soka ya nchini humo.
Maamuzi hayo yanatekelezwa mara moja, kumaanisha kwamba mechi nne za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ambazo zimeratibiwa kutandazwa Alhamisi ya Machi 10, 2022 sasa hazitaonyeshwa runingani katika taifa la Urusi ambalo linasema wanajeshi wake nchini Ukraine wanaendesha operesheni maalum.
Ilichukua muda wa dakika 15 pekee kwa suala hilo kuafikiwa katika kikao cha saa nne kilicholeta pamoja vikosi 20 vya EPL jijini London, Uingereza mnamo Machi 8, 2022.
Vinara wa EPL pia wameahidi kutoa msaada wa Sh1.5 bilioni kwa watu wa Ukraine.
Haki za kupeperusha mechi za EPL nchini Urusi zilikuwa zimepokezwa kampuni ya Rambler Group ya Urusi iliyokuwa katika mwaka wa mwisho wa mkataba wa miaka mitatu wa kuonyesha michuano hiyo moja kwa moja runingani.
Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) pia limesitisha ushirikiano wake na Urusi. Ina maana kwamba hakuna mchuano wowote wa robo-fainali ya Kombe la FA utakaonyeshwa nchini Urusi.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link