[ad_1]
Fainali ya UEFA msimu huu yahamishwa kutoka Urusi hadi jijini Paris, Ufaransa
Na MASHIRIKA
FAINALI ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu huu sasa itachezewa jijini Paris, Ufaransa baada ya Urusi kupokonywa haki hiyo baada ya kuvamia majirani zao Ukraine.
Fainali ya kipute hicho cha haiba kubwa kilikuwa awali kimeratibiwa kuchezewa jijini St Petersburg mnamo Mei 28, 2022.
Aidha, kipute cha mbio za magari ya langalanga almaarufu Formula 1 Grand Prix kilichokuwa kifanyike jijini Sochi mnamo Septemba 2022 pia kimefutiliwa mbali.
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) pia imetaka mashirikisho mbalimbali ya michezo kuahirisha au kufutilia mbali mashindano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Urusi au Belarus.
Sasa fainali ya UEFA iliyokuwa iandaliwe ugani Gazprom Arena itafanyika uwanjani Stade de France jijini Paris. Fainali ya kivumbi hicho ilifanyika jijini Porto, Ureno mnamo 2020-21 mwaka mmoja baada ya kuandaliwa jijini Lisbon, Ureno mnamo 2019-20.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
Inter Milan wapoteza fursa ya kupunguza pengo la alama kati…
[ad_2]
Source link