Connect with us

General News

Fainali za mashindano ya michezo ya vyuo vya kiufundi zafana Ndumberi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Fainali za mashindano ya michezo ya vyuo vya kiufundi zafana Ndumberi – Taifa Leo

Fainali za mashindano ya michezo ya vyuo vya kiufundi zafana Ndumberi

Na LAWRENCE ONGARO

FAINALI za mashindano ya michezo ya vyuo vya kiufundi zilifanyika katika uwanja wa Ndumberi, Kiambu mnamo Jumapili, huku wanaume na akina dada wakishiriki.

Baadhi ya vyuo hivyo ni Uthiru Vocational Training Centre, Juja Farm, Komothai, Kirangari, Nyaga, Nyanduma, Muguga, na Kinoo.

Timu ya Nyanduma VTC FC ya wanaume iliikomoa Muguga kwa mabao 4-1.

Washindi walionyesha soka safi.

Timu ya Uthiru ya voliboli kwa upande wa wanaume iliichapa Nyaga kwa seti 3-0.

Timu ya Uthiru ilionyesha mchezo wa kupendeza huku wapinzani wao Nyaga wakishindwa kabisa kujitetea vilivyo.

Timu ya Voliboli ya Uthiru VTC ilipoishinda Nyaga VTC katika fainali kwa seti 3-0. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Nayo timu ya Uthiru ya voliboli kwa upande wa akina dada iliicharaza Kirangari kwa seti 3-0.

Halafu timu ya akina dada ya netiboli ya Komothai iliichabanga Juja Farm 3-1.

Akina dada wa Komothai walifanya mshambulizi hatari katika ngome ya wapinzani wao na kuwalemea kipindi chote.

Katika uvutaji wa kamba Nyaga ilipata ushindi kwa jinsia hizi mbili za wanaume na wanawake.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Gathirwa Mugwanja alipongeza walioshiriki kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kufuata sheria za michezo.

Alisema mashindano hayo yalifana kutokana na ushirikiano mwema kati ya walimu na wanafunzi.

Mwenyekiti huyo aliwahimiza wanafunzi hao kuzingatia michezo ili kujiendeleza zaidi siku za usoni.

Maafisa wakuu waliohudhuria hafla hiyo ya michezo ni mkurugenzi mkuu, Emily Nkoroi, naibu wake Wilfred Nyarangi, na wasimamizi wengine kama Kenneth Karanja, Mary Kamau, pamoja na walimu wa michezo wa vyuo hivyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending