Connect with us

General News

Fairtrade yakusanya sahihi 1.8 milioni za wakulima kushinikiza mataifa tajiri duniani yatimize ahadi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Fairtrade yakusanya sahihi 1.8 milioni za wakulima kushinikiza mataifa tajiri duniani yatimize ahadi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi – Taifa Leo

Fairtrade yakusanya sahihi 1.8 milioni za wakulima kushinikiza mataifa tajiri duniani yatimize ahadi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Na SAMMY WAWERU

SHIRIKA la kutafutia wakulima soko la mazao la Fairtrade Africa (FTA) limekusanya sahihi 1.8 milioni za wakulima na wafanyakazi kushinikiza mataifa tajiri duniani kuafikia ahadi yao wakati wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, lililofanyika Paris 2015.

Mswada huo pia unalenga kuhimiza serikali na wadauhusika, kutoa fedha zinazopaswa kuangazia mabadiliko ya tabianchi.

Katika kongamano la Paris, viongozi wa nchi tajiri ulimwenguni waliahidi kwamba watakuwa wakifadhili mataifa yenye mapato ya chini kima cha Dola Bilioni 100 kila mwaka, kusaidia kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ahadi ambayo haijatekelezwa kufikia sasa.

Himizo la FTA limejiri wakati ambapo marais na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanaendelea na Kongamano la COP26 UN, Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Glasgow, Uingereza.

Kongamano hilo la Kimataifa, lilianza Oktoba 31 na linaendelea hadi Novemba 12.

FTA kupitia mchakato wa Be Fair With Your Climate Promise campaign, inataka viongozi wa mataifa tajiri kutekeleza haki kuafikia ahadi waliyotoa.

“Fedha hizo zinapaswa kufikia wakulima, ili kuwawezesha kupambana na mabadiliko ya hali hewa na anga,” Bi Kate Nkatha, Mkurugenzi wa Mauzo FTA akaambia Taifa Leo kupitia mahojiano ya kipekee.

Shirika hilo ni kati ya wadau katika sekta ya kilimo wanaohudhuria Kongamano la COP26, Glasgow.

FTA inalalamika, asilimia 10 ya mataifa tajiri duniani yamechangia asilimia 50 ya utoaji wa gesi hatari, nchi zenye mapato ya chini zikilazimika kubeba mzigo wa athari za machafuzi hayo ya mazingira.

“Jamii ya wakulima inayojali mazingira inaelewa athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

“Mamilioni hawana uwezo kimapato kustahimili athari hizo, jambo ambalo linahatarisha maisha yao,” Kate akaelezea.

Aidha, FTA na ambayo hufanya kazi na wakulima na wafanyakazi kote ulimwenguni inaendeleza kampeni hiyo Barani Afrika, Uingereza na Amerika.

Kupitia mswada huo itakaowasilisha Glasgow, linahimiza wanachama wake kushawishi wabunge washinikize usawa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, pamoja na ahadi iliyotolewa na mataifa tajiri kwa yenye mapato ya chini kuafikiwa.

Vilevile, linataka wabunge kuchukua hatua katika Kongamano la COP26.

Mabadiliko ya tabianchi, yanaendelea kuathiri sekta ya kilimo na ufugaji kufuatia kubadilika kwa hali ya hewa na anga, ukame ukikausha mimea na mifugo kufariki