Connect with us

General News

Familia ya msomi wa kiislamu aliyetekwa nyara sasa yamtaka Rais Kenyatta kuamuru kuachiliwa kwake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Familia ya msomi wa kiislamu aliyetekwa nyara sasa yamtaka Rais Kenyatta kuamuru kuachiliwa kwake – Taifa Leo

Familia ya msomi wa kiislamu aliyetekwa nyara sasa yamtaka Rais Kenyatta kuamuru kuachiliwa kwake

Na CHARLES WASONGA

FAMILIA ya msomi wa Kiislamu aliyedaiwa kutekwa nyara na maafisa wa polisi Alhamisi Profesa Hassan Nandwa sasa inamtaka Rais Uhuru Kenyatta kuamuru kuachiliwa kwa mpendwa wao.

Wakiongea na wanahabari katika Msikiti wa Jamia, Nairobi Jumamosi,Oktoba 30, 2021, mkewe msomi huyo Bi Mawahib na mwanawe wa kiume Elmiqdad Hassan wamejawa na wasiwasi mkuu tangu kutoweka kwa msomi huyo Alhamisi jioni.

“Tunamheshimu sana Rais wetu Uhuru Kenyatta kama kiongozi ambaye anaheshimu Katiba na sheria za nchi zinazolinda haki za rai wote. Ndio maana tunamwomba aamuru maafisa wa polisi kumwachilia huru Profesa Nandwa ili ashtakiwe rasmi ikiwa alitenda kosa lolote. Sio haki kwa maafisa wa usalama kuendelea kumzuilia,” Bi Mawahib akasema huku akibubujikwa machozi.

Mama huyo pia alitoa wito kwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i na Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kumweleza kiini cha kutekwa nyara kwa mumewe “na makosa aliyofanya.”

“Inasikitisha kuwa mume wangu alikamatwa Alhamisi jioni baada ya kuhudhuria swala ya jioni katika msikiti wa Jamia, Nairobi. Hii ni baada ya kuhudumia wateja wake na kupiga ripoti katika kituo cha Central kuhusu kukamatwa tena kwa mteja wake mwingine aliyekamilisha kifungo chake majuzi,” Bi Mawahib akaeleza.

Kwa upande wake Elmiqdad Hassan alieleza kuwa simu ya babake ilizimwa muda mfupi baada ya kukamatwa kwake sawa na akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook.

“Tulishuku kuwa mambo hayakuwa mazuri pale simu ilipozima kwa zaidi ya saa moja baada ya saa moja jioni Alhamisi. Haikuwa jambo la kawaida kwa mtu wa hadhi ya babangu kuzima simu kwa zaidi ya saa moja kwa sababu hupigiwa simu na wateja wake kila mara,” akasema.

Elmiqdad alisema baadaye maafisa saba wa polisi waliokuwa na bunduki hatari walivamia nyumbani kwao katika kitongoji cha Kingston, kando ya barabara ya Ngong.

“Walifanya msako nyumbani mwetu kwa muda wa saa moja kisha wakaondoka bila kuchukua chochote. Hata hivyo, walijitambua kuwa maafisa wa polisi na kusema kuwa walikuwa wakimsaka mwanamume mmoja ambaye aliondoka gerezani hivi majuzi,” akaeleza huku akionekana kupandwa na hisia.

Awali Jumamosi, viongozi wa kiislamu wameitaka serikali kukomesha visa vya utekaji nyara wa waumini wa dini hiyo kwa tuhuma za ugaidi.

Huku wakilaani tukio la kutekwa nyara kwa msomi wa kiislamu Profesa Nandwa, wakuu hao wa mashirika mbalimbali ya kiislamu walisema haki za Waislamu zinafaa kulindwa kwa sababu wao Wakenya.

“Serikali inafaa kukomesha hii sera ya kuchukulia Waislamu kama rais duni. Sisi ni sehemu ya raia wa nchi hii, tunachangia asilimia 30 ya Wakenya na haki zetu zinapasa kuheshimiwa sawa na Wakenya wengine” mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu Nchini (SUPKEM) Hassan Ole Naado akawaambia wanahabari.

Ole Naado aliitaka serikali kuamuru kuachiliwa huru kwa Profesa Nandwa au awasilishwe mahakamani kufunguliwa mashtaka “alifanya kosa lolote chini ya katiba na sheria za nchini hii,”

“Tunataka maafisa wa polisi waliomkamata Profesa Nandwa Alhamisi wamwasilisha kortini ili ashtakiwe kwa mujibu wa sheria ikiwa alivunja sheria kwa namna yoyote. Unyamavu huu wa polisi na serikali kuhusu suala hilo unatutia wasiwasi. Familia ya mwenzetu pia imejawa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wake,” akaeleza.

Ole Naado aliandamana na mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Waislamu (NAMLEF) Sheikh Abdullahi Abdi, mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kiislamu Nchini (CIPK), tawi la Nairobi Sheikh Athman Abdallah, Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan, Naibu Katibu Mkuu wa Kamati Simamizi ya Msikiti wa Jamia, Nairobi, miongoni mwa wengine.

Profesa Nandwa ambaye pia ni wakili mtajika alidaiwa kutekwa nyara na watu waliodaiwa kuwa maafisa wa polisi kutoka kitengo cha kupambana na ugaidi mwendo wa saa kumi na mbili za jioni.

Alikuwa ameondoka msikiti wa Jamia, Nairobi baada ya kupiga ripoti katika kituo cha polisi cha Central kuhusu kutekwa nyara kwa mteja wake, Elvis Bwire Oliacha, aliyetoka gereza kuu la Kamiti baada kukamilisha kifungo cha miaka 10 kwa kupata na kosa la ugaidi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending