Connect with us

General News

Familia yaruhusiwa kuzika mabaki ya aliyeuawa na fisi mnamo 2017 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Familia yaruhusiwa kuzika mabaki ya aliyeuawa na fisi mnamo 2017 – Taifa Leo

Familia yaruhusiwa kuzika mabaki ya aliyeuawa na fisi mnamo 2017

Na LAWRENCE ONGARO

FAMILIA moja katika kijiji cha Komo, Thika Magharibi, imepata afueni baada ya serikali kuipa idhini ya kuzika mifupa ya jamaa wao ambaye inadaiwa aliuawa na fisi Machi 2017.

Mwanamume huyo Joseph Njuguna Kamau aliyekuwa na umri wa miaka 65 wakati huo, alikuwa amepeleka ng’ombe malishoni alipovamiwa na kundi la fisi.

Baada ya kutoweka kwa siku moja, familia yake ilipata mifupa ya mikono, na sehemu nyingine huku mwili wote ukiwa umeliwa na fisi.

Frederick Kamau ambaye ni nduguye marehemu, alihutubia waandishi wa habari katika chumba cha kuhifadhi maiti mnamo Januari 6, 2022, ambapo alieleza kuwa mifugo iliyokuwa imepelekwa malishoni na nduguye ilirejea nyumbani jioni ya siku ya mkasa huo lakini nduguye, hakuonekana popote.

Alifafanua kwamba walilazimika kuishi na mabaki ya kaka yao kwa sababu serikali ilisema kuwa ni sharti ifanye uchunguzi kamili ili kubainisha kama kweli marehemu aliliwa na fisi.

Serikali ilichukua baadhi ya mifupa chache na pia kuruhusu familia hiyo kubaki na kiwango kingine.

Kulingana na Bw Kamau, maafisa wa upelelezi walitoa onyo kuwa familia hiyo isiendeshe mazishi yoyote hadi uchunguzi kamili ukamilike.

“Kwa zaidi ya miaka minne na nusu hivi, tumekuwa tukihifadhi mifupa ya ndugu yetu ndani ya nyumba ya mama yetu. Hatua hiyo imefanya mama yetu kuwa na mawazo chungu mzima na kukabiliwa na tatizo la shinikizo la damu mwilini,” alifafanua Bw Kamau akiwa na machungu moyoni.

Alisema hata mamake mzazi Bi Margaret Njeri Kamau, 95, amekuwa akingoja haki itendeke ndipo moyo wake utulie.

Hata hivyo, mnamo Januari 7, 2022 daktari bingwa wa upasuaji wa maiti Dkt Johansen Oduor alifika katika hospitali kuu ya Thika Level 5 na kufululiza hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti ili kufanyia uchunguzi wa kitaalam mifupa hiyo kubainisha ukweli wa mambo.

Kulingana na mtaalam huyo, mifupa ya marehemu ilivunjwa na meno makali ya fisi na vile vile ikabainika wazi kuwa mifupa hayo ni ya marehemu.

Hatimaye familia ya marehemu ilipata matokeo ya uchunguzi huo na ikapewa idhini ya kuzika mabaki ya mpendwa wao.

Lakini familia imeiomba serikali iwasiliane na Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) ili ilipwe fidia.

Kwa wakati huu familia inaendesha shughuli za mazishi na inatarajiwa kwamba wengi watahudhuria wakitokea sehemu za mbali.

Wiki mbili zilizopita katika maeneo ya Makongeni na Witeithie, Juja, fisi walivamia wakazi wa eneo hilo. Takriban watu wawili walivamiwa na kuuawa na fisi hao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending