Connect with us

General News

Gavana hatimaye amuunga mkono Ruto – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Gavana hatimaye amuunga mkono Ruto – Taifa Leo

Gavana hatimaye amuunga mkono Ruto

Na ALEX NJERU

GAVANA wa Tharaka Nithi, Muthomi Njuki hatimaye ametangaza kumuunga mkono Naibu Rais William Ruto kwa urais baada ya muda mrefu wa kuficha msimamo wake.

Aidha, ametangaza azma yake ya kutetea kiti chake kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Hii inamaanisha kuwa yuko tayari kumenyana na anayeonekana kuwa mpinzani wake mkuu na mwandani wa karibu wa Naibu Rais, Seneta Kithure Kindiki katika teuzi za UDA.

Akizungumza Jumatano katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Kathwana, eneobunge la Chuka/Igambang’ombe, mkuu huyo wa kaunti alisema amekuwa akijificha kwa muda mrefu na hawezi tena kuficha urafiki wake kisiasa na Naibu Rais.

“Tayari nimeashiria ninakoelekea na hivi karibuni nitaitisha mkutano kutangaza msimamo wangu,” alisema Gavana Njuki.

Kiongozi huyo wa Kaunti alipigia debe mno Mpango wa Maridhiano (BBI) na vilevile akampokea Kiongozi wa ODM, Raila Odinga katika kaunti hiyo kufanyia kampeni azma yake ya urais mwaka uliopita.

Alisema amekuwa mwandani kisiri ili watu wake waendelee kunufaika kutokana na miradi ya maendeleo kutoka kwa serikali kuu.

“Nilichukua muda ili kuhakikisha watu wangu wanazidi kupokea miradi ya maendeleo kutoka kwa serikali kuu,” alisema bosi huyo wa kaunti.