Afisa mmoja katika serikali ya kaunti ya Nairobi alifariki dunia Jumatatu, Julai 13 kutokana na virusi vya COVID-19
Nicholas Nkamasai alizikwa Jumatano, Julai 15 nyumbani kwake kaunti ya Narok chini ya masharti makali yaliowekwa na wizara ya afya ya kuzika maiti za COVID-19.
Habari Nyingine: Afisa wa kaunti ya Nairobi azikwa Narok baada ya kufariki kutokana na coronavirus
Nicholas Nkamasai alifariki dunia kutokana na ugonjwa corona.Picha: Mike Sonko/Facebook Source: UGC
Akiwa amehuzunishwa na kifo cha mmoja wa maafisa wake, Sonko amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kulichukulia janga hili la ugonjwa wa corona kimzaha.
Sonko amewataka Wakenya wachukue tahadhari zinazohitajika ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Habari Nyingine: Afisa wa kaunti ya Nairobi azikwa Narok baada ya kufariki kutokana na coronavirus
Sonko awatahadharisha Wakenya baada ya afisa wa kaunti kufariki kutokana na COVID-19 Source: UGC
” Huu ugonjwa upo, hebu na tujitahadhari, leo tumempa heshima za mwisho mmoja wa maafisa wa kaunti kule Narok,” Sonko alisema.
” Hebu na Mungu ailaze roho yake mahala pema, tunaiombea familia wakati huu mgumu wa majonzi,” Aliongezea Sonko.
Habari Nyingine: Ni Raila pekee atamuweza Ruto 2022, mchanganuzi Herman Manyora asema
Sonko awatahadharisha Wakenya baada ya afisa wa kaunti kufariki kutokana na COVID-19 Source: UGC
Kufikia sasa nchi imerekodi visa 11, 252 vya maambukizi ya virusi vya corona huku vifo vingine saba vikiripotiwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
VIDEO
Subscribe to watch new videos