[ad_1]
Hakuna niliyemfukuza atoke Jubilee, asema Uhuru
NA WINNIE ONYANDO
RAIS Uhuru Kenyatta amepinga madai kuwa aliwafukuza wanachama wa Jubilee ambao walianza kuegemea katika mrengo mwingine.
Akizungumza Jumamosi katika kongamano la wajumbe wa chama cha Jubilee, Rais Kenyatta amesema kuwa kila mmoja aliyejiondoa kwenye chama hicho walitoka kutokana na tamaa yao.
“Hakuna niliyemfukuza wala kumwambia ajiondoe kwenye chama. Tumekuwa tukifanya kazi bila tatizo na hivyo chama chetu kitaendelea kudumu,” akasema Rais Kenyatta.
Kwa upande mwingine, amesema nia ya chama hicho kujiunga na muungano wa Azimio la Umoja ni kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti ni wa amani.
Ametoa wito kwa viongozi wengine ambao wanawania nyadhifa mbalimbali waungane ili kuendeleza uchumi wa nchi.
“Nashukuru Bw Raila Odinga ambaye ameshirikiana nami katika uongozi wangu. Najua pamoja tutasonga mbele,” akasema Rais Kenyatta.
Next article
Ndoto yangu ni kuwa ngwiji kwenye sanaa-Anita
[ad_2]
Source link