Connect with us

General News

Hata akiwania urais huenda Kalonzo asiweze kulazimisha marudio ya uchaguzi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hata akiwania urais huenda Kalonzo asiweze kulazimisha marudio ya uchaguzi – Taifa Leo

CECIL ODONGO: Hata akiwania urais huenda Kalonzo asiweze kulazimisha marudio ya uchaguzi

NA CECIL ODONGO

KUYUMBAYUMBA kwa kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka kunaonyesha kuwa sababu yake ya kuwania urais ni kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Agosti 9 unaingia duru ya pili ili ang’ang’aniwe na ama Raila Odinga au Naibu Rais Dkt Willliam Ruto.

Baada ya kukosa kupokezwa wadhifa wa mgombeaji mwenza wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Musyoka aliuhepa muungano huo na kupelekea jina lake kwa Tume ya Uchaguzi (IEBC) kama mwaniaji urais wa Wiper.

Kwanza ni dhahiri kuwa nia ya Bw Musyoka ni kuwakosesha Bw Odinga na Dkt Ruto wa Kenya Kwanza karibu kura milioni mbili za eneo la Ukambani.

Anafanya hivyo akitumai kuwa akiwania urais jinsi alivyofanya 2007, jamii hiyo itaendelea kumuunga mkono na kumpigia kura kwa wingi.

Hata hivyo, huenda hilo likakosa kutimia kwa kuwa magavana Charity Ngilu (Kitui) na Prof Kivutha Kibwana (Makueni) nao wako katika mrengo wa Bw Odinga na watahakikisha kuwa anapata sehemu za kura za eneo hilo.

Kwa upande mwingine Gavana wa Machakos, Dkt Alfred Mutua, seneta wa zamani Johnstone Muthama na baadhi ya wabunge kutoka Ukambani wanaomuunga mkono Dkt Ruto pia watahakikisha anajizolea sehemu za kura za Wakamba.

Hata kama Bw Musyoka atapata kura kutoka jamii yake, kihesabu hazitawezesha kulazimisha duru ya pili iwapo Bw Odinga na Dkt Ruto nao watadumisha kura kwenye maeno ambako wana ushawishi mkuu kisiasa.

Kitakachomwangamiza Bw Musyoka zaidi ni kuwa iwapo mmoja kati ya Dkt Ruto au Bw Odinga atashinda duru ya kwanza ya uchaguzi, basi huenda akasalia kwenye baridi kisiasa kwa mara nyingine.

Kuwa nje ya serikali kutayeyusha udhibiti wa Bw Musyoka katika siasa za Ukambani kwa sababu nao viongozi wengine watakuwa wamechipuka na kuteka siasa za jamii hiyo.

Hata nafasi aliyopewa ya mkuu wa mawaziri na Bw Odinga akishinda urais ataikosa.