Connect with us

General News

Hatutaunga mwaniaji urais nje ya OKA- vinara – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hatutaunga mwaniaji urais nje ya OKA- vinara – Taifa Leo

Hatutaunga mwaniaji urais nje ya OKA- vinara

Na SHABAN MAKOKHA

VINARA wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA), wamekashifu viongozi wanaochochea ghasia na wakaapa kuwa hawatatishwa ili kuunga mgombeaji mwingine wa urais nje ya muungano wao.

Wakizungumza mjini Kakamega walipokutana na wajumbe wa vyama vyao Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper), Gideon Moi wa Kanu and Ford Moses Wetangúla wa chama cha Ford Kenya, walifichua kwamba kuna watu wenye ushawishi wanaowapigia simu wakitaka waunge mgombea wa urais nje ya OKA.

“Tupatie kila kiongozi nafasi ya kuuza manifesto yake ili Wakenya waamue kiongozi aliye na mikakati bora,” alisema Bw Mudavadi. “Hatutaruhusu yeyote atulazimishie uongozi. Hatutaruhusu yeyote kuwalazimishia Wakenya anayepaswa kuwa rais 2022.

Tumekataa simu tunazopigiwa usiku kutulazimisha kuunga mtu mmoja,” alisema. Bw Musyoka alisema vinara wa OKA hawatatusi au kuvumilia wanachama wa muungano huo wanaoshiriki vitendo vya ghasia vinavyoweza kusababisha ghasia nchini na kurudisha nyuma demokrasia.

Alipuuza mifumo ya uchumi inayotumiwa na Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kujipigia debe akisema kinachohitajika ni kupunguza ushuru unaotozwa Wakenya kwa asilimia 50.

“Tukipunguza ushuru kwa asilimia 50, uchumi utakuwa sawa na Wakenya watakuwa na pesa na kuacha kutegemea pesa chache wanazodanganywa nazo. Ajenda ya OKA ni kufufua uchumi na kuukuza pamoja na kujenga umoja na utangamano miongoni mwa Wakenya,” alisema Bw Musyoka.

Alimkashifu Katibu Mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini, Francis Atwoli na kumtaka aheshimu vinara wa OKA na kukoma kuwatusi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending