Connect with us

General News

Hofu Omicron ikienea katika nchi 89 duniani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hofu Omicron ikienea katika nchi 89 duniani – Taifa Leo

Hofu Omicron ikienea katika nchi 89 duniani

GENEVA, Uswizi

Na MASHIRIKA

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema virusi vya corona aina ya Omicron vimesambaa katika nchi 89 kote duniani kufikia sasa.

Kwenye ripoti kuhusu hali ya virusi hivyo duniani jana, shirika lilisema kiwango cha maambukizi yake kinaongezeka maradufu kati ya siku moja na siku tatu.Kulingana na tathmini ya shirika hilo, virusi hivyo vinasambaa kwa kasi katika nchi zenye watu wengi, hata ikiwa wamechanjwa dhidi ya corona.

Lilisema litatoa taarifa zaidi kuhusu virusi hivyo na sababu halisi zinazovifanya kusambaa sana, hata miongoni mwa watu waliopewa chanjo.Shirika lilitangaza virusi hivyo kuwa hatari mnamo Novemba 26, mara tu baada ya kubainika nchini Afrika Kusini.

Kufikia sasa, hakuna mengi yanayojulikana kuhusu virusi hivyo.Wanasayansi wanataja virusi hivyo kuwa hatari, ijapokuwa hawajatoa maelezo kuvihusu.Hata hivyo, uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kuwa virusi hivyo vinazidi nguvu baadhi ya chanjo na vinasambaa kwa haraka kuliko vile vya Delta. “Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusu athari za virusi aina ya Omicron.

Tunahitaji maelezo mengi kubaini kasi ya kusambaa kwake na ikiwa chanjo zilizopo zina uwezo wa kukabili makali yake,” ikasema WHO.Ijumaa, utafiti wa mwanzo uliofanywa na Taasisi ya Imperial jijini London, ulionyesha kuwa kuna hatari ya mtu kuambukizwa virusi hivyo mara tano zaidi ikilinganishwa na aina nyingine ya virusi. Tafiti pia zimeonyesha virusi ni hatari kuliko vile vya Delta.U

tafiti huo unapuuza maelezo yaliyokuwa yametolewa na wataalamu kutoka Afrika Kusini kwamba virusi hivyo si hatari kama ilivyodhaniwa awali.Utafiti huo ulitolewa na maafisa wa serikali nchini Uingereza huku taifa hilo likitangaza visa vipya 93, 045 vya maambukizi jana.

Licha ya baadhi ya wataalamu kusema athari za virusi vya Omicron si hatari ikilinganishwa na vile vya Delta, wataalamu nchini humo walisema bado hawajabaini hilo.Walisema utafiti huo ulionyesha kasi ya kuambukizwa virusi vya Omicron ni mara tano zaidi ikilinganishwa Delta.

Hata hivyo, kauli yao ni kinyume na ripoti za wanasayansi Afrika Kusini, wanaosema kuwa tafiti zao zinaonyesha athari za Omicron si hatari ikilinganishwa na za Delta.Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex, ametaja msambao wa virusi hivyo barani Ulaya kuwa na “kasi ya radi.”

Alhamisi, Rais Joe Biden wa Amerika alionya kuhusu “hatari ya maradhi hatari na vifo” kwa raia ambao bado hawajapewa chanjo dhidi ya virusi hivyo.Mawaziri wa afya kutoka mataifa saba tajiri zaidi duniani (G7) wametaja virusi hivyo kuwa tisho kubwa zaidi linaloikumba sekta ya afya duniani.

Mawaziri walitoa kauli hiyo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom kusema “virusi hivyo vinasambaa kwa kasi kubwa zaidi ikilinganishwa na aina nyingine hapo awali.”“Kufikia sasa, ni wazi hatupaswi kupuuzilia mbali athari za virusi hivi.

Ni janga hatari linaloikumba dunia nzima. Hata ikiwa virusi aina ya Omicron havina madhara makubwa kiafya ikilinganishwa na vingine, kasi ya kusambaa kwake ni ya kutia wasiwasi,” akasema Tedros.Mkurugenzi huyo alisema ilipofikia, itayalazimu mataifa husika kuwahamasisha raia wake kuchukua tahadhari zifaazo kuhakikisha wamejilinda dhidi ya athari za virusi hivyo.

“Tunaishi katika mazingira ambayo licha ya juhudi zinazoendeshwa na nchi mbalimbali, itawalazimu raia kuchukua juhudi zao wenyewe kujilinda dhidi ya maambukizi,” akasema.