Connect with us

General News

Hofu ya tishio la kuua waumini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hofu ya tishio la kuua waumini

Hofu ya tishio la kuua waumini

Na WYCLIFFE NYABERI

TAHARUKI imetanda eneo la Otamba, Kisii baada ya watu waliochoma makanisa mapema mwaka huu kutishia kuwaua waumini na wahubiri.

Jumapili, vijikaratasi vidogo vilivyokuwa vimeandikwa kwa mkono katika lugha ya Ekegusii, vilipatikana mlangoni mwa kanisa Katoliki la Mtakatifu Monika la Otamba, vikionya kuhusu maovu mbalimbali.

Vijikaratasi hivyo vilikuwa na jumbe kama hizi: “Sasa watu wa Otamba nimerudi tena. Ni mimi yule niliyekuwa nikiyachoma makanisa. Safari hii ni watu nitaua. Tayari nimekwisha malizana na mtu mmoja na namjua anayefuata kwenye laini.

Nikimaliza, nitamuua padre wa kanisa hili kwa kumroga. Atakapokufa, nitafungua kanisa langu na watu watakuja kuniabudu, la sivyo watakufa. Lazima mnigeukie la sivyo nitawageuza muanze kupigana nyinyi kwa nyinyi,” kikasema kijiratasi kimoja kilichorushwa kanisani.

Pia ameiomba serikali itoe ripoti ya uchunguzi kuhusu mioto ya kwanza. “Machifu wahakikishe ni nani anayeandika jumbe kama hizi. Jambo hili limetiwa watu woga kwa yale yaliyoandikwa na watu hao hawatoki mbali. Hii inaonyesha jinsi shetani ameanza kuingia katika maisha ya wanadamu,” padre Nyaanga akasema.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kisii Francis Kooli anasema wanachunguza jambo hilo.