Connect with us

General News

‘Hutaingia Uhuru Gardens ikiwa hujavalia barakoa’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

‘Hutaingia Uhuru Gardens ikiwa hujavalia barakoa’ – Taifa Leo

‘Hutaingia Uhuru Gardens ikiwa hujavalia barakoa’

NA CHARLES WASONGA

WALE wote wanaotarajia kuhudhuria sherehe za 59 za Madaraka Dei katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi, Jumatano, Juni 1, 2022 wameagizwa kuvalia barakoa.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Jumanne, Mshirikishi wa Ukanda wa Nairobi Kang’ethe Thuku alisema wale ambao hawatavalia vitambaa hivyo vya kuzuia maambukizi ya Covid-19 watazuiwa kuingia katika uwanja huo.

“Tunawahimiza Wakenya wanaopanga kufika katika bustani ya Uhuru Gardens wawe wamevalia barakoa ili wawe salama,” Bw Thuku akasema kwenye taarifa.

Agizo hilo la mshirikishi huyo wa Nairobi limejiri siku ambayo Katibu wa Wizara ya Afya Susan Mochache ametoa tahadhari kwa Wakenya kuhusu ongezeko la visa vya maambukizi ya Covid-19.

Amewataka warejelee mtindo wa kuvalia barakoa katika maeneo ya umma, kanuni ambayo iliondolewa mnamo Machi 11, 2022. Hii ni baada ya kiwango cha maambukizi kushuka hadi chini ya asilimia moja.

Mnamo Jumanne, Mei 31, 2022, Kenya iliandikisha kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.4 .

Mnamo Jumamosi Mei 28, 2022 kiwango cha maambukizi kilipanda hadi asilimia 5.5 na kuzua hofu ya kushuhudiwa kwa wimbi la sita la maambukizi.

Wakenya wanaopanga kuhudhuria sherehe hizo za Madaraka Dei pia wameshauriwa kuwasili katika Uhuru Gardens saa kumi na mbili alfajiri.

Serikali inasema kuwa jumla ya watu 30,000 wanatarajiwa kufika katika bustani hiyo.

Na kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa mlipuko wa Covid-19 Machi 13, 2020 sherehe hizo zitaandaliwa katika kaunti zote 47, ambapo hotuba ya Rais Kenyatta itasomwa na Makamishna wa Kaunti.