[ad_1]
Ida Odinga aomba msamaha kwa makanisa
Na CHARLES WASONGA
MKEWE kiongozi wa ODM Raila Odinga, Ida Odinga, ameomba msamaha kuhusiana na kauli aliyotoa mwishoni mwa wiki jana kwamba kuwe na sheria ya kudhibiti shughuli za makanisa nchini.
Akiongea jijini Kisumu, Mama Ida pia alipendekeza kwamba makanisa yaongozwe na wachungaji waliopokea mafunzo ya thiolojia.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Bi Odinga aliondoa ushauri wake kwa Baraza la Kitaifa la Makanisa Nchini (NCCK) kwamba liweke kanuni kali za kuongoza usajili wa makanisa mapya na kufutilia usajili wa makanisa yasiyotimiza kanuni hizo.
“Ningependa kuondoa ushauri niliyotoa kwa NCCK kwamba liweke kanuni za kudhibiti shughuli za makanisa chini yake ili kuimarisha shughuli nzima ya kueneza njili nchini,” Ida akasema kwenye taarifa kwa vyombo vya habari.
“Nimegundua kuwa kauli zangu ziliwachukiza baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali nchini. Naomba msahama kwa namna ambavyo kauli yangu iliwakera waumini wa makanisa husika,” akaongeza.
Bi Odinga alisema pendekezo lake kuhusu haja ya wachungaji kupokea mafunzo lilivumishwa mitandaoni kwa njia isiyofaa na hivyo kuonekana kuwa yenye nia mbaya.
Alisema kuwa amekuwa akithamini kazi ya kanisa na amejitolea kuchangia katika mpango wa kupiga jeki huduma ya kanisa nchini “ili kuboresha jamii.”
“Kwa miaka mingi nimeheshimu kazi za wahubiri wengine kupitia sala wanazotoa zenye uwezo wa kuboresha maisha ya wanajamii,” Bi Ida akaongeza.
Mkewe Bw Odinga, alitoa msamaha huo baada ya Wakenya kumshambulia kupitia mitandao ya kijamii kwa kupendekeza kanuni za kukandamiza makanisa.
Next article
Watu saba wafariki dunia baada ya matatu kukanyaga kilipuzi…
[ad_2]
Source link