Connect with us

General News

Ida Odinga awataka Wakenya waishi bila kurushiana cheche – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ida Odinga awataka Wakenya waishi bila kurushiana cheche – Taifa Leo

Ida Odinga awataka Wakenya waishi bila kurushiana cheche

NA MWANGI MUIRURI

MKE wa kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga, Mama Ida Odinga, Ijumaa amewataka Wakenya wajumuike ndani ya mrengo wa Azimio la Umoja ili wafurahie maana halisi ya umoja na ustawi wa kitaifa.

Alisema kuwa mwaniaji wa urais kwa mrengo huo ambaye ni Bw Raila Odinga ndiye mfaafu zaidi na ambaye atahakikishia Wakenya ufanisi huo wa kisiasa.

Akiongea katika Kaunti ndogo ya Mathioya katika Kaunti ya Murang’a alipojumuika na viongozi wengine kusambaza miche ya ndizi na miparachichi, Mama Ida alisema kuwa Bw Odinga ambaye ni mumewe ana nia njema kwa Taifa la Kenya na huwa kila kuchao anawawazia Wakenya mema.

Vilevile, aliwataka Wakenya kumheshimu Mama Ngina Kenyatta ambaye katika siku za hivi karibuni “amekuwa akilengwa kisiasa na wapinzani wa Bw Odinga.”

Hatua hiyo ya kulengwa kisiasa imechochewa na hatua yake ya kumuunga mkono Bw Odinga kuwania urais.

Bw Odinga na chama chake cha ODM amejumuika pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kuunda mrengo wa Azimio la Umoja.

Mama Ida aliteta kuwa kwa sasa wanasiasa wengi wanamkosea Mama Ngina heshima.

“Mama Ngina sio mwanamke tu hivihivi bali ni mmoja wa viungo muhimu katika historia yetu. Ningetaka kuwakumbusha Wakenya kwamba ni muhimu waheshimu kina mama.

“Sio lazima umtukane mwenzio ndio uwasilishe ujumbe wako wa kisiasa. Kumtukana Mama Ngina sio kujifaa kisiasa. Ni kujidunisha na kudunisha Taifa lako,” akasema.

Aliongeza kuwa kwa sasa kuna cheche nyingi za kisiasa anbazo zimetapakaa katika ulingo wa kisiasa, akiwaomba Wakenya na wanasiasa kuvumiliana na kuzingatia amani.

Alisema ushindani ulioko kwa sasa kisiasa sio wa kuzua chuki bali ni wa kusaka ufaafu wa kesho ya Kenya na wananchi wake.

Alisema kuwa amani ni muhimu katika msimu huu wa kisiasa na baadaye ikizingatiwa kuwa baada ya kura ya Agosti 9, kutakuwa na mitihani ya kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne.