Connect with us

General News

Idadi ya wanaomenyania ugavana Nairobi yaongezeka – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Idadi ya wanaomenyania ugavana Nairobi yaongezeka – Taifa Leo

Idadi ya wanaomenyania ugavana Nairobi yaongezeka

NA DANIEL OGETTA 

IDADI ya wanaogombea kiti cha ugavana katika Kaunti ya Nairobi imeongezeka baada ya mfanyabiashara Agnes Kagure kutangaza rasmi azma yake kabla ya Uchaguzi Mkuu Agosti.

Awali, Bi Kagure alikuwa ametangaza atawania wadhifa huo kupitia tiketi ya Jubilee. Idadi ya wanawake wanaogombea ugavana Nairobi sasa ni watatu wakiongozwa na gavana wa sasa Anne Kananu, Askofu Margaret Wanjiru.

Johnson Sakaja atakayewania kupitia tiketi ya ANC amefanya jumla ya wanaomezea mate afisi ya ugavana katika jiji kuu kutimia wanne.

Bi Kagure aliyezindua kampeni yake jana katika Kasarani Indoor Arena, vilevile alitaja ajenda tano anazonuia kutekeleza ili kuboresha maisha ya wakazi jiji kuu.

Iwapo atawahi kiti hicho cha ugavana, mfanyabiashara huyo ameahidi kupunguza msongamano wa trafiki jijini kwa kufanyia mageuzi sekta ya usafirishaji wa umma, kuimarisha usalama jijini na kuunda nyadhifa mpya za kazi 200,000 kila mwaka katika muda wa miaka mitano ijayo.

Aidha, alisema kuwa ana mipango ya kuboresha usambazaji wa maji, usafi na huduma za afya kwa wakazi wote jijini ikiwemo kupanua viwanda na nafasi za biashara.

“Nataka kujitolea maisha yangu kuboresha Nairobi na kuwahamisha kutoka jiji la kuomboleza hadi katika jiji la kushangilia. Baada ya kuishi karibu katika kila kona ya jiji hili, ninaweza kuwaelewa kabisa,” alisema Bi Kagure.