Connect with us

General News

IEBC kuchunguza madai ya Ruto kuwa kuna njama ya wizi wa kura – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

IEBC kuchunguza madai ya Ruto kuwa kuna njama ya wizi wa kura – Taifa Leo

IEBC kuchunguza madai ya Ruto kuwa kuna njama ya wizi wa kura

NA ERIC MATARA

HUENDA Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) ikamwamrisha Naibu Rais Dkt William Ruto afike mbele yake kutokana na madai aliyoyatoa ziarani Marekani kuwa kuna mipango ya kuiba kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema tume hiyo itachunguza madai hayo kama sehemu ya mikakati yake ya kuhakikisha kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

“Binafsi sijapata maelezo ya kina kuhusu madai aliyoyatoa Naibu Rais Dkt William Ruto akiwa Marekani.

Baada ya kupata maelezo, IEBC itachunguza madai hayo kisha kutoa ufafanuzi kwa Wakenya,” akasema Bw Chebukati akiwa jijini Nakuru.

“Wawaniaji wote wa urais wanafaa kutii sheria. Tutachunguza suala hili na kuwaeleza Wakenya kuhusu madai ya wizi wa kura,” akaongeza Mkuu huyo wa IEBC.

Alizungumza baada ya IEBC kutia saini mkataba na washikadau katika sekta ya uanahabari wa jinsi ya kufuatilia matukio kabla wakati na baada ya uchaguzi huo. Hasa mkataba huo utajikita katika kuhakikisha vyombo vya habari vinaeneza kwa kuchapisha au kutangaza habari zilizothibitisha kuhusu uchaguzi huo.

Dkt Ruto alitoa madai kuwa kuna mipango ya kushiriki udanganyifu mnamo Jumanne akiwa Marekani ambapo alitoa wito kwa umoja wa

mataifa uingilie kati na kuzuia jaribio la udanganyifu katika uchaguzi huo.

Hasa Naibu Rais alisema kuwa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta inahusika kwenye mpango huo wakati akitoa hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Loyola, Maryland. Alithibitisha madai yake kwa kudai kuwa idara mbalimbali za serikali sasa zinatumika kuwatishia na kuwakandamiza viongozi wanaomuunga mkono.

Dkt Ruto anayeongoza muungano wa Kenya Kwanza na Chama cha UDA, atakabiliana na Kinara wa ODM Raila Odinga wa vuguvugu la Azimio la Umoja miongoni mwa wagombeaji wengine katika uchaguzi huo.

Madai kuwa kuna mipango inayoendelea ya wizi wa kura yaliyotolewa na Dkt Ruto hata hivyo yalijibiwa vikali na wandani wa Bw Odinga ambao walisema hiyo ilikuwa ishara kuwa Naibu Rais alikuwa ametambua atashindwa katika uchaguzi huo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending