Connect with us

General News

IEBC yalazimika kuahirisha kikao cha kusikiliza kesi inayomkabili Sabina Chege – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

IEBC yalazimika kuahirisha kikao cha kusikiliza kesi inayomkabili Sabina Chege – Taifa Leo

IEBC yalazimika kuahirisha kikao cha kusikiliza kesi inayomkabili Sabina Chege

NA WINNIE ONYANDO

TUME ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) imeahirisha kikao cha kusikiliza kesi inayomkabili Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Murang’a, Sabina Chege, baada ya wakili aliyekuwa akimwakilisha katika kesi hiyo kuthibitisha kuwa amelazwa katika hospitali ya Nairobi.

Kesi hiyo ambayo ilifaa kuendelea leo Jumanne sasa imeahirishwa hadi Machi 8, 2022.

“Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8,” akasema Mwenyekiti wa IEBC Bw Wafula Chebukati.

Wakili wa mwanasiasa huyo, Otiende Amallo ameeleza paneli ya IEBC kuwa Bi Chege hangeweza kufika kutokana na hali yake ya kiafya.

Hii ilikuwa awamu ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Tume hiyo ilimwamrisha Bi Chege afike mbele yake baada ya matamshi yake yaliyoashiria kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa 2017 ambapo Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuendelea kuwatumikia Wakenya kwa muhula wa pili.