[ad_1]
IEBC yaokoa madiwani
NA COLLINS OMULO
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewahakikishia madiwani wanaopania kuwania nyadhifa za juu katika uchaguzi mkuu ujao kwamba hawatahitajika kujiuzulu kama watumishi wa umma.
Hii ni baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kuwataka madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya chama cha Democratic Party (DP), na wanaotaka kuwania nyadhifa za juu, kujiuzulu. Bw Muturi ambaye ni kiongozi
wa chama hicho alisema madiwani hawa hawataidhinishwa kuwania viti hivyo ikiwa hawatajiuzulu.
Huku akirejelea kipengele cha 99 (2) (d), Spika huyo alisema madiwani anaomezea mate viti vya ubunge, ugavana, useneta au urais huenda wakazimwa kuwania wakifeli kutimiza hitaji hilo Hata hivyo, jana, Bw Chebukati alifafanua kuwa sheria inawahitaji madiwani kujiuzulu tu kabla ya kuwasilisha karatasi zao za uteuzi kwa maafisa wa kusimamia uchaguzi.
Mwenyekiti huyo alisema suala hilo lilishughulikiwa kotini ambapo Mahakama Kuu mnamo Mei 2021.
[ad_2]
Source link