Connect with us

General News

Ithibati za kiisimu kwamba kuna Kiswahili na Viswahili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ithibati za kiisimu kwamba kuna Kiswahili na Viswahili – Taifa Leo

KAULI YA PROF IRIBE: Ithibati za kiisimu kwamba kuna Kiswahili na Viswahili

Na PROF IRIBE MWANGI

NIMEULIZWA swali hili mara kwa mara lakini kila wakati mimi hujibu kwamba ni Kiswahili na Viswahili.

Ni Kiswahili kwa kuwa ni lugha inayojisimamia.

Ni lugha yenye sauti zake, msamiati wake na miundo yake. Ni lugha kwa kuwa ina jamii inayoitumia kama lugha yake asilia na ya kwanza.

Ni lugha pia kwa kuwa kuna jamii ambayo inajiita “Waswahili” na inayotumia lugha inayoitwa “Kiswahili.”

Jamii hii ina utamaduni, itikadi na mwonoulimwengu sawa.

Ni lugha kwa kuwa inakidhi vigezo vyote vya kuainisha lugha.

Kama lugha iliyokua, Kiswahili kimepata vilugha vyake. Kwa lugha sanifu, vilugha hivi huitwa lahaja.

Lakini je, lahaja katika Kiswahili zimetokana na nini? Kuna sababu tatu muhimu zilizozaa lahaja za Kiswahili.

Sababu ya kwanza ni umbali wa kiwakati. Umbali huu umezaa lahaja ya Kale au ya Kihistoria. Lahaja inayotajwa zaidi hapa ni Kingozi ambacho hasa huitwa “Kiswahili cha kale.”

Mbali na wakati, kuna umbali wa kijiografia au kimaeneo. Umbali huu umesababisha kuwepo kwa lahaja nyingi za Kiswahili kulingana na mahali kinapozungumzwa. Mswahili wa Lamu atazungumza lahaja za Lamu kama vile KiAmu na KiTikuu ilhali yule wa Pemba atazungumza lahaja za Pemba kama vile KiTumbatu na KiHadimu.

Hatimaye kuna lahaja zinazotokana na “umbali” wa kijamii. Umbali huu unaweza kuwa wa kiuchumi (matabaka) au hata wa kiumri ambapo kila kundi katika jamii linazungumza ‘Kiswahili’ chake.

Kutokana na ithibati hizi basi, ni sahihi kusema kwamba kuna Kiswahili na Viswahili.