Connect with us

General News

Itumbi asimulia masaibu yake mikononi mwa watekaji nyara – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Itumbi asimulia masaibu yake mikononi mwa watekaji nyara – Taifa Leo

Itumbi asimulia masaibu yake mikononi mwa watekaji nyara

Na WANGU KANURI

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidijitali katika Ikulu, Dennis Itumbi ameelezea yaliyomsibu alipotekwa nyara na watu wasiojulikana katika eneo la Thindigua, Kaunti ya Kiambu mwaka 2021.

Kupitia kwa kurasa za akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook, Bw Itumbi alidai kuwa upande anaoegemea kisiasa ulikuwa sababu kuu ya yeye kudhulumiwa alipotekwa nyara.

“Lazima ubadilishe ushawishi wako wa kisiasa ili uafikiane na bosi,” akasimulia.

Alipouliza huyo bosi alikuwa nani, alizabwa kofi, akagongwa teke huku pingu zikikazwa kama alivyoeleza.

“Magari mawili yaliendeshwa kwa kasi huku nikiwa pahali penye miti, giza na mvua nyingi iliyokuwa ikinyesha. Nilikuwa na soksi tu. Singeweza kuketi chini sababu uchungu niliokuwa nikihisi mwilini ulikuwa mwingi na hata singeweza kuyafungua macho yangu,” akasema.

Hali kadhalika, Bw Itumbi aliyesaidiwa na mwendeshaji teksi Bw Boniface Makokha, alisema dereva huyo alimfaa kwa kumpa shuka la kujifunika kwa sababu aliachwa akiwa uchi.

Pia alimpongeza kwa kumnunulia soda kisha kumpeleka hospitalini.

“Nakuvulia kofia Boniface Makokha,” ujumbe ukasema.

Amesimulia haya siku chache baada ya mshirika huyo wa karibu wa Naibu Rais William Ruto kutangaza kuwa atawafichua waliomteka nyara.

Licha ya kukiri kuwa alikwisha wasemehe waliomteka nyara, Bw Itumbi alisema kuwa atatangaza kanisani waliomteka nyara Februari.

Akizungumza aliporuhusiwa kuenda nyumbani baada ya kulazwa kwa siku kadhaa, Bw Itumbi alieleza kuwa bado hajatikisika kisiasa.

“Sitishiki na imani yangu kwa mrengo wa Hasla haijabadilika,” akasema.

Kulingana na ushuhuda uliotolewa na mashahidi, mwanablogu huyo alitekwa nyara na watu watatu waliovalia mavazi ya kawaida alipokuwa akitoka kwenye kinyozi kimojawapo.

Hata hivyo, baada ya habari ya utekwaji nyara wake kusambaa, Wakenya na wanasiasa walikashifu vikali kitendo hicho huku wakimshukuru Mungu kwa Bw Itumbi kuwa hai.

Hali kadhalika, Wakenya waliibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hatua iliyoifanya Idara ya Polisi kueleza kuwa ilikuwa ikifanya uchunguzi kubaini kilichofanyika.

Kupitia kwa Msemaji wa Polisi Bruno Shioso, idara hiyo iliomba Wakenya kuwa na utulivu huku akiwataka wasieneze uvumi.