Jamaa wawili wanaswa na polisi kwa madai walikuwa wanaeleka Somalia kujiunga na al-shabaab. Picha: NPS. Source: UGC
Mahakama iliarifiwa kuwa wawili hao hawakupiga ripoti katika afisi za uhamiaji kwamba walikuwa wanaelekea Somalia.
Ripoti za polisi zinaonesha kuwa Wesonga na Odhiambo waliondoka Mumias kuelekea Mandera Oktoba ambapo walikodisha chumba kwa muda wa mwezi moja kabla ya kuvuka boda.
Inashukiwa kuwa wawili hao walikuwa wanaelekea eneo la Baidoa kujiunga na kundi la al-shabaab kwani walipowasili Bulahawa walikodisha teski ya kuwalekeza eneo hilo.
Washukiwa walinaswa na majeshi ya Somalia ambayo yaliwakabidhi kwa majeshi ya Kenya yanayopambana na ugaidi.