Jamaa alimuua mkewe Jumapili, Juni 15 mtaa wa Kiganjo mjini Thika na kisha akajisalimisha kwa polisi siku moja baadaye.
Mshukiwa Stephen Gikuhi Mwirigi mwenye umri wa miaka 30 alimuua mkewe Bakita Njeri kwa kile polisi wanashuku huenda ilikuwa ni mzozo wa nyumbani Nairobi News iliripoti.

Jamaa amuua mke kisha akajisalimisha kwa polisi. Picha: UGC.
Source: Depositphotos
Taarifa iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Makongeni, kaunti ya Kiambu chini ya OB 20/15/6/2020 ilifichua kuwa Mwirigi alifanya kitendo hicho na kutorokea Tana River kabla ya kujisalimisha kwa polisi.
Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi Mary Wanjiku ambaye ni mpwa wake marehemu baada ya kupashwa kuhusu tukio hilo na maafisa wa kituo cha Madogo.
“Aliarifiwa kuwa mjomba wake alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Madogo na alikiri kumuua mkewe majira ya saa 11 jioni,” taarifa ya polisi ilisema.

Taarifa iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Makongeni ilifichua kuwa Mwirigi alifanya kitendo hicho na kutorokea Tana River kabla ya kujisalimisha kwa polisi.
Source: UGC
Polisi kutoka Makongeni kisha walikimbia hadi eneo la tukio na kupata mwili wa mama huyo ukiwa juu ya kitanda huku shingo lake likiwa limefunikwa kwa kitambaa.
Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Thika Level kufanyiwa upasuaji.
Kwa sasa mshukiwa angali anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Madogo akisubiri kuhamishwa hadi kituo cha Makongeni.