Connect with us

General News

Jambojet yaanzisha uchukuzi wa mizigo hadi Goma, DRC – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jambojet yaanzisha uchukuzi wa mizigo hadi Goma, DRC – Taifa Leo

Jambojet yaanzisha uchukuzi wa mizigo hadi Goma, DRC

NA MARY WANGARI

JUHUDI za kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Kenya na mataifa jirani zimepigwa jeki baada ya Shirika la Ndege la Jambojet kuzindua rasmi usafirishaji mizigo nchini na Bara Afrika kwa jumla.

Shirika hilo ambalo ni tawi la Kenya Airways (KQ) vilevile limeanzisha mkondo mpya wa kusafiri – sha mizigo kutoka jiji kuu la Nairobi hadi jiji kuu la Goma, Mashariki mwa taifa DR Congo (DRC).

Jambojet sasa itakuwa ikitumia ndege zake aina ya Dash 8-Q400 kusafirisha mizigo kupitia vituo vyake vinane nchini ikiwemo Nairobi, Kisumu, Eldoret, Mombasa, Ukunda, Malindi, na Lamu.

Akizungumza jana katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Sarova Panafric, Nairobi, kwa niaba ya Waziri Msaidizi Betty Maina, Waziri Msaidizi David Osiany alipongeza hatua hiyo akisema ilitokana na mkataba uliotiwa saini majuzi kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Rais Felix Tshisekedi.

“Usafirishaji mizigo ni moja kati ya shughuli zinazozalisha mapato ya kiwango cha juu zaidi Barani Afrika.

Kwa kuzindua mkondo huu, Jambojet itachangia pakubwa kurahisisha uchukuzi wa mizigo na kupanua biashara kati ya Kenya na Goma DRC,” alisema Bw Osiany.

Mkurugenzi wa Jambojet Karanja Ndegwa alifafanua kuwa shirika hilo litatumia vituo vyake sita kusafirisha mizigo kama vile mazao, bidhaa za kimatibabu, mizigo ya kawaida na hata usafirishaji wa miili.

“Wateja wanaotaka kusafirisha mizigo baina ya vituo vyetu nchini watalipa kuanzia Sh5,109, Sh6,813 na Sh7,948 kwa mizigo yenye uzani wa kuanzia kilogramu 45 kwenda juu, kilogramu 100 kwenda juu na kilogramu 250 kwenda juu mtawalia,” “Mizigo itakayosafirishwa kutoka Nairobi hadi Goma yenye uzani wa chini ya kilogramu 45 itatozwa Sh11,355,” alisema Bw Ndegwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kukabiliana na Bidhaa Ghushi, Bi Florah Mutahi alisema.

Uzinduzi wa Jambojet umejiri mwezi mmoja tu baada ya kupata idhini kusafirisha mizigo katika maeneo mbalimbali nchini na mataifa jirani, kwa kutumia ndege zake za abiria.