[ad_1]
KCSE 2021: Jeriel Ndeda Obura kutoka Mang’u High aibuka mtahiniwa bora kitaifa
NA CHARLES WASONGA
JERIEL Ndeda Obura wa Mang’u High School, ndiye aliyeibuka mwanafunzi bora kitaifa katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE 2021 akiwa na A ya pointi 87.167, matokeo yanaonyesha.
Akitangaza matokeo hayo, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amebainisha kwamba ni watahiniwa 826,807 waliofanya KCSE 2021 ikiwa idadi ya juu ukilinganisha na 747,000 waliofanya KCSE 2020. Ni ongezeko la asilimia 10.66.
Aidha, Watahiniwa 1,138 walipata A ambapo 349 ni wa kike nao 789 wakiwa wa kiume.
Obura alifuatwa na Mukuha Timothy Kamau wa Shule ya Upili ya Alliance aliyepata alama 87.139 huku Job Ngara wa Shule ya Upili ya Mang’u akipata alama 87.1 na kushikilia nambari ya tatu.
Katika nafasi hiyo ya tatu pia walikuwepo Chege David Kamau wa Shule ya Upili ya Wavulana ya St Joseph, Kitale (87.1) na Ramadhan Musa Tepo wa Light Academy (87.1).
Mtahiniwa Mwendo Sicily Mutheu wa Kenya High ndiye alishikilia nambari nne kwa kupata alama 87.086 huku Ian Mwai Toyota wa Kakamega High akiwa wa tano kwa kupata alama 87.08.
Arita Shekinah wa Kenya High alishikilia nambari sita kitaifa kwa kupata alama 87.079 huku Musindi Daniel Ouma wa Light Academy akiwa wa saba kwa kupata alama 87.0.
Mtahiniwa Brenda Cherutich wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis pia alishikilia nambari saba kwa kupata alama hiyo hiyo ya 87.0.
Wengine waliopata alama hiyo ni; Mugane Job Ngatia wa Strathmore School, Pretie Ariona Adanga wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Kapsabet, Mutethia Caleb (Shule ya Upili ya Mang’u), Abiyah Melania Nelima (Kenya High) na Maina Millicent Wamuru (Kenya High).
Next article
Timu ya Ruto yaahirisha kampeni Kenya ikiomboleza Kibaki
[ad_2]
Source link