Connect with us

General News

Jinsi wakazi wa Nairobi walivyosherehekea Krismasi bila ‘lockdown’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi wakazi wa Nairobi walivyosherehekea Krismasi bila ‘lockdown’ – Taifa Leo

Jinsi wakazi wa Nairobi walivyosherehekea Krismasi bila ‘lockdown’

Na SAMMY WAWERU

BAADHI walisafiri mashambani na wengine kusalia mijini na majijini, taswira inayoshuhudiwa kila mwaka msimu wa Krismasi.

Ni msimu unaosherehekewa na Wakristo ulimwenguni kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu japo kuna baadhi wenye mitazomo kinzani kuhusu tarehe ya kuzaliwa kwake. Makala haya hayajikiti kwa huo mjadala.

Krismasi ya mwaka huu, 2021 ilikuwa ya pili Wakenya kuiadhimisha chini ya mikakati ya Wizara ya Afya (MoH) ya kudhibiti janga la Covid-19.

Ugonjwa wa Covid-19 na ambao kwa sasa ni janga la kimataifa, ulitua nchini Machi 2020.

Huku baadhi wakisafiri mashambani kujumuika na jamaa zao, waliosalia mijini walienjoi Krismasi kwa staili.

Mwanamume aliyekunywa pombe kupindukia katika mojawapo ya barabara jijini Nairobi, Krismasi 2021. PICHA | SAMMY WAWERU

Aidha, kuna walioenda mashinani Sikukuu hiyo iliyoangukia Jumamosi, sawa na waliowatangulia wakipokezwa mjeledi wa nauli ghali.

Kwa mfano, waliosafiri Nyeri na Nakuru, hawakuwa na budi ila kugharamia ada ya Sh500, masafa ambayo kwa kawaida huwa wastani wa Sh300.

Walioenda Nanyuki na Meru, walifukua mfuko zaidi ya Sh1, 000 kinyume na nauli kati ya Sh500 – 700 wanayolipa.

“Hatuna msimu mwingine wa kuvuna vinono mbali na huu,” mhudumu mmoja wa matatu akaambia Taifa Leo, katika steji ya Tea Room, jijini Nairobi.

Licha ya kituo hicho kuonekana kikiwa na idadi ndogo ya abiria mnamo Jumamosi, alisema siku iliyotangulia nauli ilikuwa mara dufu.

Katika barabara ya Tom Mboya, na ambayo hushuhudia msongamano wa watu na magari, Krismasi shughuli za usafiri zilionekana kupungua.

Taswira hiyo haikuwa tofauti na ya Luthuli Avenue.

Hayo yakijiri, wengine walitumia maadhimisho hayo kupiga mtindi kupita kiasi wakionekana kulemewa na makali ya pombe na kukata kiu cha usingizi barabarani.

Baa na maeneo ya burudani licha ya kuhimizwa kuwa makini, mashabiki wa pombe walifurika humo na kujivinjari bila kujali mikakati na kanuni za wizara za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Hayo yalidhihirika wazi kupitia uchunguzi wa Taifa Leo katika baadhi ya vilabu eneo la Zimmerman, kiungani mwa jiji la Nairobi.

“Ni vigumu kudhibiti mtu aliyelewa,” akasema mhudumu wa baa inayofahamika kama Jubilee, aliyejitambua kwa jina Wairimu.

Kwa wale ambao hawakusafiri mashambani wala kuwa katika maeneo ya burudani, walisherehekea Krismasi kwenye mabustani, wengine wakiwa ama kazini au nyumbani wanakoishi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending