Connect with us

General News

Jinsi ya kuandaa mayai ya kukoroga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi ya kuandaa mayai ya kukoroga – Taifa Leo

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa mayai ya kukoroga

Na MARGARET MAINA

[email protected]

PROTINI zilizoko ndani ya mayai kando na kuujenga mwili pia hukufanya kutohisi njaa haraka.

Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda mrefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.

Muda wa matayarisho: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 3

Mayai kabla ya kuvurugwa. PICHA | MARGARET MAINA

Vinavyohitajika

  • Mayai 6
  • Pilipili mboga 1
  • Nyanya 2
  • Kitunguu maji 1
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta ya kupikia kiasi
  • Maziwa robo kikombe
  • Nyanya ya kopo
  • Jibini
Mayai ambayo yanavurugwa. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Katakata viungo vyote na weka kwenye vyombo tofauti. Koroga mayai yako yawe tayari kupikwa.

Weka kikaangio mekoni baada ya kuwasha jiko. Ongeza mafuta vijiko viwili, weka chumvi kiasi, kisha ongezea vipande vya vitunguu maji, na ukoroge mpaka viive na kuwa rangi ya kahawia.

Ongeza pilipili mboga na koroga mchanganyiko wako kisha weka nyanya na endelea kukoroga mpaka nyanya iive na kutengeneza kama rojo flani.

Weka mayai huku unayakorogakoroga, na kabla hayajakauka, ongeza maziwa na uendelee kukoroga.

Ongeza nyanya ya kopo kidogo, koroga, na malizia kwa kuweka jibini.

Koroga mchanganyiko huo mpaka uive vyema. Pakua mayai tayari kwa kuliwa.