Connect with us

General News

Jinsi ya kuandaa wali wa ‘kabsa’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi ya kuandaa wali wa ‘kabsa’ – Taifa Leo

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa wali wa ‘kabsa’

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 50

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • Mchele 1 ½ kikombe
  • Vipande vikubwavikubwa vya kuku
  • Mafuta ya kupikia kikombe 1
  • Vitunguu 2 vya maji
  • Nyanya 4 zilizokatwakatwa
  • Nyanya ya kopo kijiko 1
  • Karoti mbili zilizoparwa
  • Tangawizi mbichi iliyosagwa – kijiko ½
  • Maganda ya chungwa yaliyosagwa nusu kijiko
  • Ndimu iliyokaushwa
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga nusu kijiko
  • Iliki iliyosagwa nusu kijiko
  • Mdalasini nusu kijiko
  • Karafuu iliyosagwa kijiko 1 ¼
  • Njugu za lozi
  • Zabibu kiasi

Maelekezo

Tayarisha sufuria yako na uibandike kwenye meko ya moto wa wastani.

Mimina mafuta ya kupikia na uhakikishe yamepata moto. Tia vitunguu maji vilivyokatwakatwa na tangawizi iliyosagwa na uanze kukoroga hadi vibadilike rangi.

Mimina maganda ya machungwa yaliyosagwa, pilipili manga, iliki, ndimu, mdalasini, na karafuu katika mchanganyiko huo kisha weka nyanya ya kopo na uendelee kukoroga.

Funika ili nyanya zivurujike na ziive.

Osha vipande vya kuku kisha uvitumbukize kwenye viungo vyako ulivyovikaanga. Koroga kwa dakika tatu kisha mimina maji lita moja kwenye mchanganyiko huo na kuacha nyama ya kuku iive kwa dakika 15.

Toa kuku kwenye ule mchuzi kwa kutumia kijiko. Panga vipande vya kuku kwenye ovena na uhakikishe moto utakaotumia ni wa kiasi.

Osha mchele vizuri kisha mimina kwenye ule mchuzi na ukoroge.

Chukua kareti ulizopara na umimine pia, ukiwa bado unakoroga angalia kiini cha wali na hakikisha umeiva.

Funika wali wako na upunguze moto kwa kiasi ili upishi wako uendelee taratibu.

Weka mafuta kwenye kikaangio na yakipata moto, mimina lozi zako ulizozichambua huku ukikoroga hadi ziwe kavu kabla ya kuepua mafuta. Chukua zabibu pia uzikaange na baadaye uzitoe na uziache zipoe.

Upishi wa kabsa utakua umekamilika na unaweza ukapakua. Baadaye utaongezea lozi na zabibu kwa juu pamoja na kuku baada ya kutoa kwenye ovena.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending