[ad_1]
Joho asema Raila ana timu ya kumfanyia kampeni aingie Ikulu
NA WINNIE ONYANDO
GAVANA wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ni mmoja wa viongozi wanaomfanyia kampeni kinara wa ODM, Raila Odinga amemhakikishia Rais Uhuru Kenyatta kuwa Bw Odinga ataibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.
Akizungumza Jumamosi katika kongamano la wajumbe wa ODM jijini Nairobi, Bw Joho alisema kuwa yeye pamoja na timu yake watahakikisha kuwa Bw Odinga ameshinda katika uchaguzi huo.
Alimwomba Rais Kenyatta aondoe wasiwasi kwa kuwa “hakuna atakayemshinda Bw Odinga.”
“Leo nakuahidi Rais kuwa ni Bw Odinga ndiye atakayeibuka mshindi. Yeye ndiye anayefaa kukurithi,” akasema Bw Joho.
Alisema kuwa yeye na kamiti yake inayojumuisha gavana wa Machakos, Alfred Mutua, Junet Mohamed, gavana wa Kilifi, Amason Kingi, Kanini Kega na wengineo watahakikisha kuwa Bw Odinga ameingia ikuluni.
[ad_2]
Source link