Connect with us

General News

Jubilee wafuta alama za Ruto talaka ikikamilika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jubilee wafuta alama za Ruto talaka ikikamilika – Taifa Leo

Jubilee wafuta alama za Ruto talaka ikikamilika

ELVIS ONDIEKI Na JUSTUS OCHIENG

CHAMA cha Jubilee kimefuta alama ya ushirikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Wake William Ruto katika nembo yake mpya.

Chama hicho kimeondoa rangi nyeusi na manjano ambazo zimekuwa zikihusishwa na kilichokuwa chama cha URP, alichoongoza Dkt Ruto kati ya 2013-2016.

Nembo ya zamani ya chama cha Jubilee ambayo sasa imebadilishwa. PICHA | MAKTABA

Pia, mchoro wa mkono wa Rais na naibu wake wakisalimiana umeondolewa.

Isitoshe, kauli mbiu ya ‘Tuko Pamoja’ imebadilishwa na sasa kinajivumisha kwa kauli ‘Mbele Pamoja’.

Rangi za manjano na nyeusi zilikuwa za URP ambayo ilivunjwa wakati wa kubuniwa kwa chama cha Jubilee kuelekea uchaguzi wa 2017.

URP ilikuwa kwenye muungano na The National Alliance (TNA) katika uchaguzi wa 2013 ambayo pia ilivunjwa 2016 wakati zaidi ya vyama 10 viliungana kubuni Jubilee.

Nembo mpya ya Jubilee ambayo ina rangi nyeupe na nyekundu pekee tayari imepelekwa kwa Taasisi ya Kitaifa ya Kuhifadhi na Kusajili Nembo (KIPI) ili isajiliwe ndipo isitumiwe na chama kingine.

Baada ya kuwasilisha rangi ya nembo hiyo mpya kwa KIPI, kisheria inatarajiwa kuwa yeyote ambaye anapinga matumizi yake ana hadi Februari 2022 kuwasilisha malalamishi huku Jubilee ikiweka mikakati ya kujiimarisha kuelekea 2022 baada ya wanasiasa wa mrengo wa Dkt Ruto kujiondoa.

Pia, kudumishwa kwa nembo ya njiwa ambayo ilikuwa kwenye ile ya awali na kuifanya iwe maarufu zaidi miongoni mwa wafuasi wa Rais na Naibu wake inaonyesha wazi kuwa, Jubilee imeamua kuondoa alama zozote zinazohusishwa na URP.

Naibu Katibu Mkuu wa Jubilee, Joshua Kutuny jana Jumamosi alieleza Taifa Jumapili kuwa, chama hicho kimeweka mikakati ya kuendelea kujifufua na kitakuwa na sura mpya kabisa wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2022.

Bw Kutuny alisema baadhi ya wanasiasa wanaoegemea mrengo wa Dkt Ruto wameshaamua kuondoka chamani na kujiunga na UDA na Jubilee lazima sasa ianze safari ya kujijenga upya ili kusalia na uungwaji mkono wake wa zamani.

“Ni mwanzo mpya kwetu na kwa kuwa chama hiki lazima kisalie baada ya wenzetu kuondoka, lazima sasa tujitathmini na kuanza safari ya kujijenga upya. Hatutaki kuwachanganya wafuasi wetu,” akasema Bw Kutuny.

“Baadhi ya rangi ambazo tumeondoa ni za chama kilichokuwa kikiongozwa na watu ambao tushatalikiana nao kisiasa. Na ukitazama kwa makini, baadhi ya rangi za vyama vyao vipya zilikuwa rangi za chama chetu,” akaongeza.

Alifichua kuwa pia watasaka nembo mpya kurithi nafasi ya njiwa baadaye.

Aidha, alifichua kuwa mchakato wote wa kuhakikisha chama kina nembo mpya na hakihusishwi tena na mrengo wa Dkt Ruto, utakamilika katikati ya mwezi ujao kisha uzinduzi ufanyike.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending