Connect with us

General News

Jubilee yamteua Ngatia kupambana na Wanyonyi ugavana Nairobi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jubilee yamteua Ngatia kupambana na Wanyonyi ugavana Nairobi – Taifa Leo

Jubilee yamteua Ngatia kupambana na Wanyonyi ugavana Nairobi

NA WINNIE ONYANDO

KINYANG’ANYIRO cha kiti cha ugavana jijini Nairobi huenda ikaongeza uhasama kati ya chama cha Jubilee na ODM. Hii ni baada ya chama cha Jubilee kumteua rasmi mfanyabiashara Richard Ngatia kugombea kiti hicho.

Viongozi wengine wanaowania kiti hicho ni Mbunge wa Westlands, Tim Wanyonyi ambaye atawania kupitia chama cha ODM na gavana wa sasa wa Nairobi,  Anne Kananuambaye anatetea kiti chake.

Akizungumza baada ya kumkabidhi Bw Ngatia stakabadhi zake, Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee, Jeremiah Kioni alisema kuwa chama cha Jubilee kitahakikisha kuwa Bw Ngatia amepewa tikiti ya kuwania kiti hicho kupitia muungano wa Azimio la Umoja.