Connect with us

General News

Juve Queens yalenga kutinga ligi kuu miaka mitano ijayo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Juve Queens yalenga kutinga ligi kuu miaka mitano ijayo – Taifa Leo

Juve Queens yalenga kutinga ligi kuu miaka mitano ijayo

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Juve Queens ni kati ya vikosi vya wasichana vinavyojipanga kushiriki kampeni za kuwania taji la Nairobi West Regional League (NWRL) msimu mpya.

Kocha wake, Davies Ikocheli amesema kuwa wamejifunza mengi baada ya kushiriki ngarambe kwa mara ya kwanza msimu uliyopita. Aidha anakiri kuwa hakuna kizuri hupatikana rahisi lazima wajitume kwa udi na uvumba kukabili wapinzani wao kwenye mechi za kinyang’anyiro hicho.

”Itakuwa mara ya pili kushiriki kipute hicho ambapo ninaamini watakuwa tumeiva kukabili wapinzani wetu,” alisema na kuwaomba wachezaji wake wazidi kushiriki mazoezi kujiandalia michuano hiyo. Anadokeza kuwa hawatakuwa na la ziada ila tujitume kwa udi na uvumba kuhakikisha wamebeba ubingwa wa taji hilo na kujikatia tiketi ya kufuzu kushiriki Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza.

Kwenye kampeni za msimu uliyopita wasichana hao chini ya nahodha, Mercy Achieng walijitahidi kadiri ya uwezo wao na kufanikiwa kumaliza katika nafasi tano bora. Nahodha huyo anasema kuwa katika mpango mzima wana hofia wapinzani wao wenye uwezo wa muda mrefu ikiwamo Beijing Raiders baada ya Uwezo Queens kuibuka malkia msimu uliyopita na kusonga mbele.

Naibu kocha, Collins Tiego anasema wamepania kunoa makucha ya wachezaji wengi angalau wafaulu kuchezea timu ya Harambee Starlets miaka ijayo. ”Timu za mashinani ndizo hukuza wachezaji wengi ambao baadaye hujiunga na vikosi vya Ligi Kuu ya Kenya (KWPL).

Timu ya Juve Queens inayojiandaa kushiriki mechi za kipute cha Nairobi West Regional League (NWRL)…Picha/JOHN KIMWERE

Anasema wamepania kujituma kwa udi na uvumba kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano ijayo watakuwa wamefuzu kupandishwa ngazi kushiriki ligi kuu. Kadhalika anaeleza kuwa ukosefu wa ufadhili umeibuka donda sugu ambapo huchangia timu nyingi kuvunjika na kupelekea wachezaji wengi kukosa mwelekeo maishani.

Kwenye jitihada za kijisuka kocha huyo anasema wamepandishwa wachezaji sita kutoka timu ya chipukizi ili kuwaongezea nguvu kwa mechi za msimu mpya. Anatoa wito kwa wachezaji wanaokuja nyakati zote kutia bidii kunoa vipaji vyao kwa kuzingatia michezo imeibuka ajira kama zingine.

”Michezo mbali mbali ikiwamo soka kati ya mingine imeajiri wengi wanaume na wanawake,” akasema na kuongeza kuwa kikosi kinatosha mboga kutoa mchezaji wa kimataifa miaka ijayo Doreen Nabwire. Wanasoka wengine ambao wameunda kikosi hicho ni:

Valerie Akinyi, Fiona Elizabeth, Alice Wanjiku, Issene Guyo, Ann Nyaboke, Mercy Achieng, Esther Juma, Cherop Milka, Valerie Awiti, Wanjiku Muriuki na Sheba Ligeyi. Pia wapo Wanjiku Ndumba, Mercy Aluoch, Waithera (Serah), Millicent Okello, Keturah Ligeyi, Truphena Awuor, Esther Wangeci, Pauline Nafula, Monica Michael,

Jordana Majisu, Anita Kuruna, Aluanga Whitney na Nadya Fahmy.