Connect with us

General News

Kamishna mpya ataka matumizi bora ya mali ya umma – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kamishna mpya ataka matumizi bora ya mali ya umma – Taifa Leo

Kamishna mpya ataka matumizi bora ya mali ya umma

NA KNA

KAMISHNA mpya wa Kaunti ya Mombasa, Bw Lukas Mwanza, ametoa wito kwa idara za serikali na taasisi nyinginezo kutumia vyema rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na wakuu wa idara na mashirika ya umma katika jengo la Uhuru na Kazi mnamo Jumatatu, Bw Mwanza alisema serikali ya kitaifa imetenga rasilimali tele za kujenga na kuboresha miundomsingi muhimu pamoja na miradi mingine ya maendeleo katika mji huo na nchini kwa jumla.

“Lazima sisi kama wawakilishi wa serikali tuhakikishe kuwa rasilimali ambazo zimenuiwa kwa utekelezaji wa miradi hii zimetumiwa ipasavyo,” akasema.

Kamishna huyo alichukua nafasi ya Bw Gilbert Kitiyo, ambaye alihamishwa hadi Kaunti ya Makueni katika mabadiliko yaliyotangazwa na serikali hivi majuzi.

Alitaka pia wakuu wa taasisi za umma wahamasishe wananchi kuhusu miradi inayoendelezwa na serikali ya kitaifa ili kuepusha uenezaji wa habari za uongo kuhusu serikali hasa mitandaoni na majukwaa mengine.