[ad_1]
WANDERI KAMAU: Kampeni ya serikali kuongeza kiwango cha misitu nchini ni nzuri
Na WANDERI KAMAU
WAKATI wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani, Jumatatu, ilidhihirika kuwa kiwango cha misitu nchini kwa sasa kimefikia asilimia nane ikilinganishwa na mwaka 2000 ambapo kiwango cha misitu nchini kilikuwa asilimia 1.7 pekee.
Kulingana na wataalamu wa mazingira, kupungua kwa kiwango cha misitu kumechangiwa na mioto na ukataji miti ambao umekuwa ukiendelezwa na watu wanaobuni makazi mapya au maeneo ya kukuza chakula.
Hata hivyo, tangazo la Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko kwamba Kenya inaendelea kupiga hatua kwenye juhudi za kuongeza kiwango chake cha misitu ni jambo la kutia moyo.
Kwa mara ya kwanza, ni wazi serikali imeonyesha juhudi za kuongeza kiwango cha misitu tangu Bw Tobiko ateuliwe waziri.
Ingawa bado kuna visa vya mioto vinavyoendelea kuripotiwa katika sehemu tofauti nchini, ni wazi juhudi za serikali zinadhihirika. Baadhi ya misitu ambayo serikali imehusika pakubwa kuiboresha ni Mau, Mlima Kenya, Aberdares, Mlima Elgon kati ya mingine.
Katika msitu wa Mau, baadhi ya hatua ambazo serikali imechukua ni kutwaa maeneo yaliyokuwa yakikaliwa na watu kinyume cha sheria.
Katika msitu wa Aberdares, serikali imekuwa ikiendesha juhudi za upanzi wa maelfu ya miche katika maeneo yaliyochomeka au miti ilikatwa na watu kinyume cha sheria.
Licha ya hatua hizi, serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kuziendesha bila kujali athari za watu wanaotolewa katika maeneo walimokuwepo.
Wito mkuu kwa serikali ni kuwa licha ya mafanikio makubwa iliyopiga, ijali athari zake kwa wenyeji wa maeneo husika.
[email protected]
Next article
Raila aidhinisha Fernandes Barasa awe mrithi wa Oparanya…
[ad_2]
Source link