Connect with us

General News

Karagumruk ya Shikangwa yalima Hakkarigucu inayoajiri Mkenya mwingine Mwanahalima – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karagumruk ya Shikangwa yalima Hakkarigucu inayoajiri Mkenya mwingine Mwanahalima – Taifa Leo

Karagumruk ya Shikangwa yalima Hakkarigucu inayoajiri Mkenya mwingine Mwanahalima

NA GEOFFREY ANENE

WASHAMBULIZI Jentrix Shikangwa na Mwanahalima Adam kutoka Kenya wamekutana kwenye Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake ya Uturuki ambapo wenyeji Fatih Karagumruk wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Hakkarigucu, Jumapili.

Mabao ya Karagumruk, ambayo ilinyakua Shikangwa kutoka Vihiga Queens mwezi Januari mwaka huu, yamefungwa na Mkenya huyo aliyekamilisha pasi kutoka kwa Bassira Toure na Saratou Traore.

Shikangwa alikuwa amesuka pasi zilizoishia kuwa mabao wakati Karagumruk ilipepeta Dudullu 2-0 katika mchuano uliopita mnamo Machi 19.

Alipiga picha na Adam baada ya mchuano wa hivi punde ambao mabao yote yalipatikana katika kipindi cha pili. Adam alijiunga na Hakkarigucu kutoka Thika Queens mwezi Oktoba 2021. Shikangwa na Adam ni wachezaji muhimu wa timu ya taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Starlets.

Mkenya mwingine anayecheza Uturuki ni Christine Nafula. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na klabu ya Kayserispor wiki mbili zilizopita kutoka Vihiga Queens.