Connect with us

General News

Karibu mwaka mpya wa siasa na vioja vya uchaguzi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karibu mwaka mpya wa siasa na vioja vya uchaguzi – Taifa Leo

DOUGLAS MUTUA: Karibu mwaka mpya wa siasa na vioja vya uchaguzi

Na DOUGLAS MUTUA

POKEA salamu za mwaka mpya.

Huu, hata ingawa siwi mtabiri, utapendeza ajabu! Tayari unasisimua, tayari ninaupenda, ninakuhakikishia utaupenda pia.

Haya si maandishi ya kukupa matumaini tu; kamwe sijahitimu kuwa mshauri-nasaha. Hiyo kazi ni ngumu sana. Wanaoifanya kwa dhati ya nyoyo zao ninawavulia kofia.

Kwa nini mwaka huu 2022 unaonekana kama utasisimua? Ndio mwaka wa uchaguzi mkuu tuliousubiri kwa takriban miaka minne iliyopita.

Wanasiasa watakuwa wanasarakasi, hadhira mimi na wewe. Basi tafuta gunia zima la njugu-karanga tufurahie vituko vyenyewe.

Tayari kule United Democratic Alliance (UDA) kunatokota baada ya kada na mfadhili aliyejaaliwa mafedha tele, Bi Wangui Ngirici, kuondoka huko huku akipiga ukemi.

Si ukemi tu, amewaambia wakazi wa Kirinyaga wakitaka wanaweza kumchagua Bw Raila Odinga, Bw Musalia Mudavadi au Dkt William Ruto kama rais!

Tamko hilo pekee linachangamsha, kusisimua na hata kuwaudhi wengi. Kisa na maana? Siku hizo, Ngirici alipokuwa na ukuruba na Dkt Ruto, orodha hiyo ingekuwa tofauti. Mwanzo haingekuwapo kwa maana hamna orodha ya mtu mmoja: Dkt Ruto. Mama mtu hangemtaja Dkt Ruto katika sentensi moja na Bw Odinga.

Katika ulimwengu wa kisiasa wa Bi Ngirici, Bw Odinga na Bw Mudavadi hawakuwapo kabisa. Labda wahusika wa kufikirika katika sarakasi ya kufikirika asiyocheza mtu halisi, Dkt Ruto.

Sasa mambo yamebadilika, Bw Odinga na Mudavadi wamepata uhai kamili, sikwambii hata wanaruhusiwa kushindana na Dkt Ruto! Bi Ngirici ni mbunifu kweli! Anawaua na kuwafufua anaotaka, na anatarajia wafuasi wake wote katika jimbo la Kirinyaga wamfuate pasi kuuliza hata swali moja.

Yaani swali kama ‘una akili razini wewe?’ au ‘kati yako na sisi, ni nani asiye nazo? Hayo ni maswali muhimu ya wanasiasa na wafuasi wao kuulizana, lakini wafuasi ni waoga.

Lakini hivyo ndivyo ulivyo ulingo wa siasa, wanasiasa hujifanyia watakavyo. Ajabu, mimi nawe hatuna la kusema.

Tunawafuata kama mbuzi machinjioni, hadi kichwa chini ya bendera!

Kwa hivyo, swali muhimu na sahihi kuuliza ni iwapo mpiga-kura ana akili au uji ndani ya fuvu lake.

Subiri uone hali itakavyokuwa mwaka huu hadi tutakapofanya uchaguzi hapo Agosti; wanasiasa tunaotarajia wawike katika chaguzi mbalimbali watazimwa na vinara wa vyama.

Vyeti vya kuwania chaguzi kwa vyama vikuu vitauzwa waziwazi, wanasiasa maarufu watalia hadharani, kura zitaibwa, wanasiasa maarufu watahangaishwa.

Kisha? Mimi nawe tutasubiri karaha yenyewe iishe, tutii amri ya ‘bwana mkubwa’ atakayekuwa tayari ametia kibindoni mabilioni haramu!

Vipi? Kwa kumchagulia wahuni ambao watakuwa wamepitia mlango wa nyuma na kupata tiketi za chama kwa njia haramu humu wanasiasa tulionuia kuchagua wakichezwa.

Hebu tazama kioja cha Bi Ngirici; yule mama aliyefadhili na kutetea UDA wakati Rais Uhuru Kenyatta alipomtishia yeyote aliyethubutu kujinasibisha na Dkt Ruto. Bi Ngirici alisimama kidete na kuwakabili vikali waliojaribu kumtukana Dkt Ruto, miongoni mwao Bi Anne Waiguru ambaye amesababisha Bi Ngirici kukimbia UDA.

Pindi tu Bi Waiguru alipohisi kwamba wakazi wa Kirinyaga waliwachangamkia sana wanasiasa waliojihusisha na Dkt Ruto, aliisha mirindimo ya matusi.

Kufumba na kufumbua, alitangaza wazi kwamba angejiunga na UDA, eti amsaidie Dkt Ruto kutimiza ndoto yake ya kuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya. Alipokelewa upesi, tena kwa taadhima, matusi aliyotema siku zile yakanuka kama mawaridi yaliyochunwa asubuhi ya leo, Bi Ngirici akaanza kuenguliwa polepole.

Kumbuka ni yuleyule Waiguru aliyesemekana kubeba mabilioni ya pesa za ufisadi kwa magunia, Dkt Ruto akamtukana na kumkejeli hadharani.

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending